Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lionel Messi

Lionel Messi ambaye ni raia wa Argentinandiye anaongoza kuvuta pesa ndefu. Messi akiwa na miaka alikwenda Hispania baada ya Barcelona kukubali kumlipia gharama za matibabu. Nyota huyo hadi sasa amekubali kuongeza mkataba wake ambapo atasalia hadi msimu wa mwaka 2020/21.
 
Cristiano Ronaldo

Jarida la Forbes limemtaja Ronaldo kama mchezaji wa pili aliyelipwa pesa ndefu mwaka 2028 akiwa amejikusanyia kitita cha Dola 61 milioni. Ametengeneza takribani Dola 47 milioni huku akivuna jumla ya Dola 108. Mafanikio hayo aliyapata akiwa mchezaji wa Real Madrid.
 
Neymar

Nyota huyo anayekipiga PSG kwa sasa amekuwa akitambulika zaidi kwa jina lake la kwanza Neymar.

Ni mchezaji wa tatu ghari akikusanya Dola 90 milioni. Anatengeneza Dola 73 milioni kutokana na mshahara wake huku akitengeneza kiasi kingine cha 17 milioni kutokana na mkataba wake.
 
Paul Poba

Ni mchezaji wa tano anayelipwa pesa nzuri duniani. Anatengeneza Dola 29.5 milioni which inajumuisha Dola 25 milioni anazopata kutokana na mshahara huku akiwa na salio la Dola 4.5 milioni kwa mujibu wa mkataba wake.
 
Hakuna jipya hapo. Yote aliyoyasema, kwa namna moja au nyingine, hayajaanza leo wala jana na yanahusiana na tapo la Kifalsafa lijulikanalo kama Existentialism. Tapo hili lilianzishwa na mwanafalsa wa Denmark aliyejulikana kama Soren Kierkegaard. Huyu jamaa alilalamika sana kuhusu ugumu wa maisha na akamuuliza Mungu kwa nini hakuulizwa kabla ya kuzaliwa? Kwa nini Mungu Alidhani kuwa kila mtu aliyezaliwa alitaka kuzaliwa? Alisema safari ya binadamu inayoanza kwa kulia na kumalizika kwa kuliliwa haina furaha wala amani isipokuwa maumivu tu na mahangaiko na akashauri binadamu atafute suluhisho kwa Mungu ambaye ndiye pekee anayeelewa hasa kusudi la kuwepo kwa binadamu.

Mawazo haya ya Soren Kierkegaard hasa kuhusu dhana ya kumuona Mungu kama kimbilio yalipingwa vikali na mwanafalsafa wa Kijerumani aliyeitwa Friedrich Nietzsche. Huyu alidai kwamba Mungu Asingeweza kuwa suluhusho la mateso ya binadamu kwa sababu Mungu Alikuwa Amekufa. Mwaka 1882 aliutangazia ulimwengu kuwa God is Dead!. Alichomaanisha ni kwamba dhana nzima ya uwepo wa Mungu ina maluweluwe na wanaojifanya kuwa ni wafuasi wake wamejaa unafiki na hawazingatii misingi ya huyo Mungu wao. Kwamba kama kweli Mungu Angekuwa hai katika mioyo yao basi wasingekuwa wanatenda waliyokuwa wanatenda. Aliishia kudai kuwa ukombozi wa binadamu kutokana na mateso yake katika maisha haya aliyolazimishwa kuyaishi bila kuulizwa unategemea juhudi zake za kibinafsi za kujitafutia furaha na ridhiko; na kamwe asiingiliwe katika juhudi zake hizi hasa kama havunji sheria. Alishambulia sana taasisi za kijamii karibu zote akidai kuwa lengo lake kuu lilikuwa ni kumnyoosha binadamu ili aendelee kuteseka vizuri na kuufisha ule upekee wake ambamo hasa ndimo mna angalau unafuu wa maisha. Ukombozi wa binadamu umo katika kujitambua yeye mwenyewe na kuishi maisha yaliyoangaziwa...

Baadaye mwanafalsa wa Kifaransa aitwaye Jean-Paul Sartre aliyafafanua kwa undani mawazo ya Kierkegaard na Nietzsche na kulipanua tapo la Existentialism kwa kuongezea mawazo na mapendekezo mengi kuhusu jinsi binadamu anavyoweza kujinasua na mateso hasa anapopambana na hali yake. Anadokeza kwamba ile kuzaliwa tu ni tragedy pengine kubwa kuliko zote katika maisha ya mtu; na maisha si kingine bali ni mlolongo wa mateso na maumivu ambayo hitimisho lake hufikia siku ya kifo. Kama Nietzsche alisema kuwa Mungu na dini haviwezi kumsaidia binadamu kuondokana na mateso haya sana sana tu vitamsahaulisha mateso hayo kwa muda kama ganzi au dawa za kupunguza maumivu zinavyompa ahueni mgonjwa kwa muda tu. Binadamu inabidi atafute ahueni katika nafsi yake kwa juhudi za makusudi za kujitambua huku akijua malengo yake hasa ni nini.

Ukiangalia vyema, huu ndiyo msisitizo mkubwa wa dini nyingi za Mashariki ya Mbali mf. Uhindu, Ushinto na zinginezo. Hizi zimekwenda mbali zaidi na kudai kuwa hakuna kifo bali kifo ni mzunguko tu wa kawaida wa kimaumbile na binadamu ana uwezo wa kuutawala mzunguko huu kama akijitambua na kuishi maisha yenye utambuzi na yasiyo na ukinzani dhidi ya nguvu zingine za kimalimwengu. Katika urazini na roho ya binadamu kuna siri zote kuhusu ulimwengu huu na malimwengu mengine na binadamu anapaswa kufanya juhudi za makusudi ili kuijua siri hii. Hii ndiyo siri itakayomfanya aondokane na hofu, Ubinafsi (mf. wa kujirundikia mali), woga, hasira, maumivu, kukata tamaa na mambo mengine mabaya yanayomhangaisha na kuyafanya maisha yake yasiwe na furaha. Roho ya binadamu haifi na huzaliwa tena na tena katika maumbo mbalimbali kutegemea na kiwango cha utambuzi na maisha iliyoishi katika maisha yaliyopita. Na kwa kuondoa kifo dini hizi zinamwondolea binadamu mojawapo ya tukio mojawapo la kutisha sana katika maisha yake. Na kama hakuna kifo, hofu, hasira, maumivu, wasiwasi, kukata tamaa na mambo mengine mabaya yanatoka wapi?

Nikipata muda nitaandika kauzi kuelezea vizuri Existentialism kwa muktadha wa kazi za Euphrase Kezilahabi - kazi ambazo ili kuzielewa sawa sawa inabidi uielewe misingi yote 7 ya Existentialism.

Kwa hivyo ukiona ishu kama hizi wala usivunjike moyo. Mambo haya hayajaanza leo wala jana; na pengine ni vizuri vijana wetu wakawa na mawazo ya aina hii kama hatimaye yatawawezesha kufikia kwenye hitimisho lisilo na shaka; na siyo chuki na kukata tamaa. Wasiwasi wangu ni elimu tunayowapa hawa watoto. Sina uhakika kama inawaandaa kuweza kufikiri kwa mapana na kwa kina kuhusu masuala haya mazito. Tena siku hizi tumepuuzia masomo ya sanaa na tunataka watoto wetu wote wawe wanasayansi. Tumesahau kwamba hata katika akademi za akina Plato na Pythagoras; japo mkazo ulikuwa ni kwenye sayansi hasa Hisabati, wanafunzi pia ilibidi wasome baadhi ya kazi kuu za kifasihi, Lojiki na Public Speaking. Kwa njia hii ndiyo unaweza kujenga jamii ya watu wanaofikiri sawa sawa na wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja.
Aiseeee hili gazeti loooteee la andjul duh
 
Back
Top Bottom