Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyota huyo alifunga bao la ushindi dhidi ya Bournemouth wikiendi wakishinda 1-0 na kufanya Man City ijikite kileleni kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miezi miwili. “Kila mtu anafahamu nini cha kufanya, ninaamini mambo yatakwenda sawa,” alisema.
 
KOCHA wa mpito wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer hawezi kurudi katika nyumba yake ya Pauni 4 milioni huko Cheshire kwa kuwa nyota wa Liverpool Virgil van Dijk amepanga.
 
Ole Gunnar Solskjaer kwa sasa anatafuta nyumba katika Jiji la Manchester, ingawa anayo moja huko Cheshire, aliyokuwana nayo tangu akiichezea Manchester United, lakini Van Dijk ndio kikwazo chake.
 
Wakati akiwa mchezaji wa Man United aliishi kwenye nyumba hiyo ya vyumba vitano lakini wakati alipokwenda Norway kuinoa Molde aliamua kuipangisha na sasa tangu aanze kuinoa Man United Desemba mwaka jana Solskjaer inamlazimu kutafuta eneo jingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…