Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwanini watu huudhika wazazi wao wanaposhirikisha umma picha zao?
La kushangaza , watoto hata hawaruhusiwi kusajiliwa na huduma nyingi za mitandao ya kijamii hadi wanapotimiza umri wa miaka 13 - hii ikimaanisha kuwa watoto wanaofuata sheria hushituka sana wanapojipata wako mtandaoni.
 
Konrad Iturbe, mwenye umri wa miaka 19 mtengenezaji wa programu ya kompyuta ya software kutoka Uhispania amasema alikuwa na "mshituko mkubwa alipokuwa na umri wa miaka 14" alipogundua kuwa wazazi wake wamekuwa wakituma picha zake mtandaoni.
 
Kusema ukweli sipendi picha zangu ziwekwe mtandaoni kwa njia yoyote - situmi picha zangu kwenye ukurasa wangu wa Instagram - kwa hiyo nilipomfuatilia mama yangu na kuona picha zangu kwenye utambulisho wake, nilimwambia nilimwambia ' aziondoe, sikukupatia ruhusa '."
 
Sonia Bokhari, mwenye umri wa miaka 14 raia wa Marekani pia alikumbwa na hali kama hiyo alipojiunga na mitandao ya Twitter na Facebook.
Katika simulizi yake kwenye Jarida la Fast Compay alisema: "Nilipoona picha ambazo mama yangu amekuwa akituma kwenye Facebook kwa miaka , nilijihisi kuaibika sana na nikahisi nimesalitiwa sana.
 
Pale kwa kila mtu kuangalia kwenye akaunti yake ya Facebook ya umma,kilikuwa ni kipindi cha aibu cha utoto wangu : barua niliyoandika nikiwa na umri wa miaka mitano, picha zangu nikilia nilipokuwa mchanga , na hata picha nilizopigwa tulipokuwa mapumzikoni nikiwa na miaka 12 na 13 ambazo sikuzifahamu ."
 
4afbda76d8a8042d7ae918b4813daa7a.jpeg
 
Back
Top Bottom