Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakuna mechi hata moja waliyoenda kucheza ugenini halafu nyavu zao zisiguswe. Nadhani hakuna timu ambayo ina rekodi kama hiyo msimu huu.”
 
Mbappe 20, aliukwaa ubingwa wa dunia mwaka jana akiwa na miaka 19 na mpaka sasa amefunga mabao 103 katika michuano yote tangu alipoanza soka na Pele anaona kwamba mchezaji huyo akinyoosha goti atafika mbali.
 
Mwaka jana Mbappe, alikuwa mchezaji wa pili mwenye umri mdogo kufunga katika fainali za Kombe la Dunia baada ya Pele. Alifunga bao wakati Ufaransa ilipoimaliza Croatia kwa mabao 4-2 kwenye mchezo wa fainali na kiwango chake kilimkuna Pele ambaye sasa haoni ni kitu gani kinaweza kumzuia asifanikiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…