Kwenye Ligi Kuu England timu zilizofungwa mabao mengi zaid ugenini ni Fulham waliochapwa 44, wakifuatiwa na Bournemouth waliofungwa 37, kisha Huddersfield wamefunga 35, halafu Burnley mabao 31, Brighton 30, Cardiff City na Southampton wamefunga mabao 28 kila mmoja kisha wanafuata Arsenal na Watford waliofungwa mabao 27. Manchester United na Chelsea zimefungwa idadi sawa, mabao 24, huku Tottenham na Everton wao wakigungwa mabao 21, huku Wolves wakiwa na rekodi tamu kuliko vigogo ya kufungwa mabao 19.