Kilichopo ni kwamba kwenye mechi zao saba walizobakiza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, tano wanacheza ugenini. Mechi zao za ugenini walizobaki Arsenal kwenye ligi msimu huu wakianzia na Everton baadaye leo, watakuwa na kibarua pia cha kuwavaa Watford, Wolves, Leicester City na Burnley. Mechi zao mbili za nyumbani, watawakabili Crystal Palace na Brighton.