Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aisee sio kwa kukata tamaa huko..
sasa kama hawatabadilika unashaurije? nini kifanyike?
Siyo kukata tamaa. Ndiyo ukweli (japo ni mchungu). Tunalo tatizo sisi Waafrika. Haiwezekani karibia bara zima tuwe na matatizo yanayofanana fanana. Ubinafsi wa kutisha. Huu unazaa ufisadi usioisha. Hatuna hata dhana ya legacy....

Kuhusu masuluhisho, kuna machapisho mapya ya Dambisa Moyo na Ngugi yameeleza kwa ufasaha sana kinachopaswa kufanyika. Tatizo ni utekelezaji ... na hakuna short cut. Kubadili mtazamo na falsafa ya jamii ya watu inachukua muda. Pengine siku moja....

Afrika adui yetu mkuu, kwa maoni yangu, ni huu ufisadi usioisha. Ukiangalia vizuri hata hizi ishu nyingine za kuminya demokrasia na mengineyo mzizi wake unakwenda huko huko kwenye ufisadi. Na kuutokomeza/kuupunguza ufisadi huu ndiyo mtihani wetu mkubwa.
 
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]sio kweli,mpole sana
Jana tulikuwa tunapiga stori na washikaji hapa nikakutumia kama mfano wa kutoamini watu wanaojifanya wapole na wastaarabu. Ulipokuja hapa yaani ulikuwa mpole balaa. Heri ningejua kuwa utageuka na kuwa "adui" nambari wani wallahi ningeanza kukunyanyasa na Shiro wako asubuhi na mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…