Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane wala hana presha, amekuwa na uhakika mkubwa kwamba atanasa huduma ya staa huyo wa zamani wa Lille ili akakipige kwenye kikosi chake huko Bernabeu.
Hazard mwenyewe alisema: “Real Madrid ni klabu bora duniani na hiyo imekuwa ndoto ya siku nyingi tangu nilipokuwa mdogo.”
Kwa hasabu hizo, Hazard atakuwa akipokea kama Pauni 350,00 kwa wiki kwa mkataba huo wa miaka sita na kuzidi kiwango kile ambacho Chelsea wanataka kumpa cha Pauni 300,000 kwa wiki ili abaki London. Msimu huu, Hazard amefunga mabao 17 na kuasisti mara 12 katika mechi 41 alizocheza katika michuano yote.