Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shida iliyomwondoa Ramsey kwenye kikosi cha Arsenal ni kushindwa kuafikiana juu ya mazungumzo ya mkataba mpya upande wa mshahara ambapo Juventus wamekubali kumpa staa huyo Pauni 400,000 kwa wiki na kwenda kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa ndefu kwenye Serie A.
 
Kiwango chake anachokionyesha kwa sasa bila ya shaka anataka kutufanyia kitu kimoja muhimu. Anataka kutusaidia kufanya kitu fulani kwa sababu anahisia na Arsenal na anawapenda mashabiki wake," alisema Emery.
 
Hesabu ziko hivi, kwamba Los Blancos, wamepanga kumpa Hazard mkataba wa miaka sita ambao utawagharimu Pauni 110 milioni, lakini pia watawalipa Chelsea ada yao ya uhamisho ya Pauni 100 milioni na kwamba pamoja kunafanya dili zima la kumnasa staa huyo wa Kibelgiji kugharimu Pauni 210 milioni.
 
Tangu wiki iliyopita ilidaiwa kwamba dili hilo linaweza kutangazwa muda wowote ule baada pande zote kufikia makubaliano. Hazard anaweza kuondoka Stamford Bridge bure kabisa ikifika mwakani kama Chelsea haitakuwa imemuuza kwenye dirisha lijalo la uhamisho au kumsainisha mkataba mpya.
 
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane wala hana presha, amekuwa na uhakika mkubwa kwamba atanasa huduma ya staa huyo wa zamani wa Lille ili akakipige kwenye kikosi chake huko Bernabeu.
Hazard mwenyewe alisema: “Real Madrid ni klabu bora duniani na hiyo imekuwa ndoto ya siku nyingi tangu nilipokuwa mdogo.”
Kwa hasabu hizo, Hazard atakuwa akipokea kama Pauni 350,00 kwa wiki kwa mkataba huo wa miaka sita na kuzidi kiwango kile ambacho Chelsea wanataka kumpa cha Pauni 300,000 kwa wiki ili abaki London. Msimu huu, Hazard amefunga mabao 17 na kuasisti mara 12 katika mechi 41 alizocheza katika michuano yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…