Kocha Emery anaweza kushawishika kumpiga bei Xhaka, ambaye aliigharimu Arsenal Pauni 30 milioni ili kupata pesa zaidi za kufanya matumizi kwenye dirisha likalo.
Kocha huyo Mhispaniola ameambiwa kwamba kama anataka kuwa na pesa zaidi ya kiasi cha Pauni 45 milioni atakazopewa kusajili basi atapaswa kuuza baadhi ya wachezaji asiowahitaji kwenye kikosi chake mwishoni mwa msimu huu ili kupata mkwanja utakaotosha kufanya usajili wa mastaa wengine anaowataka. Moja ya wachezaji wanaosakwa na Arsenal ni Nicolas Pepe wa Lille.
NI fitina au kitu gani? kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ameibuka katika mazoezi ya timu yake hiyo ya zamani na kisha akasafiri na timu hiyo mpaka Hispania kwa ajili ya pambano la leo la marudiano la robo-fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Barcelona.
Ferguson ambaye mara mbili aliwahi kucheza dhidi ya Barcelona katika pambano la fainali michuano hiyo, ameongozana na kijana wake, Ole Gunnar Solskjaer nchini Hispania kwa ajili ya kujaribu kufanya maajabu ambayo wote waliyafanya miaka 20 iliyopita katika uwanja wa Nou Camp.
Solskjaer alikuwa mchezaji chini ya Ferguson na alifunga bao la ushindi katika mechi ya maajabu ya fainali hizo dhidi ya Bayern Munich katika uwanja wa Nou Camp ambapo United wanatarajia kujaribu maajabu hayo kwa kuichapa Barcelona ambayo ilipata ushindi wa bao 1-0 Old Trafford wiki moja iliyopita.
Alipoulizwa kama ana uwezo wa kurudia maajabu kama hayo, Solskjaer ambaye alifunga bao moja na jingine kufungwa na Teddy Sheringham katika pambano hilo la mwaka 1999 alisema “Siamini katika maajabu, lakini naamini unakipata ambacho unastahili. Kuna mambo yanakuwa yamepangwa kama ukipambana sana.”
Katika safari hiyo, bosi mtendaji wa zamani wa Manchester United, David Gill ambaye ni rafiki wa karibu wa Ferguson naye alisafiri kwenda Hispania akiwa amefuatana na Ferguson baada ya wote kuhudhuria kwanza mazoezi ya timu hiyo.
Katika safari hiyo mastaa, Nemanja Matic na Alexis Sanchez ambao afya zao zilikuwa zinasuasua katika siku za karibuni wanatazamiwa kusafiri lakini kuna uwezekano mkubwa kiungo wa Hispania, Ander Herrera asiwepo katika safari hiyo.
Licha ya kufungwa bao 1-0 katika uwanja wao wa nyumbani Jumatano iliyopita, United wamekuwa wakijipa moyo kutokana na matokeo waliyopata katika pambano la mtoano dhidi ya PSG ambapo walifungwa mabao 2-0 nyumbani lakini wakashinda mabao 3-1 ugenini.
Kwa upande wa Barcelona, kuelekea katika pambano hilo kocha wao, Ernesto Valverde Jumamosi katika pambano dhidi ya Huesca aliwapumzisha mastaa wake watano wakiongozwa na staa wa timu hiyo, Lionel Messi.
Wengine waliopumzishwa katika pambano hilo lililomalizika kwa sare ya bila kufungana ni pamoja na mshambuliaji pacha wa Messi, Luis Suarez pamoja na mlinzi, Gerard Pique na viungo, Sergio Busquets na Ivan Rakitic.
Katika pambano la awali, Messi aliondoka uwanjani akiwa na maumivu baada ya kugongwa na mlinzi wa United, Chris Smalling na kutokwa damu nyingi puani, lakini kocha wake, Valverde amedai kwamba staa huyo wa kimataifa wa Argentina yuko fiti kwa ajili ya mechi ya leo.
Niliongea naye na yuko poa, lakini aligongwa kwa nguvu sana. hakujisikia vizuri wakati mechi ikiendelea na siku moja baada ya mechi. Ilikuwa kama vile amegongwa na treni.” Alisema kocha huyo.
Niliongea naye na yuko poa, lakini aligongwa kwa nguvu sana. hakujisikia vizuri wakati mechi ikiendelea na siku moja baada ya mechi. Ilikuwa kama vile amegongwa na treni.” Alisema kocha huyo.
Pambano jingine la robo fainali leo ni kati ya Juventus na Ajax Amsterdam baada ya pambano la kwanza baina ya timu hizo mbili kumalizika kwa sare ya 1-1 nyumbani kwa Ajax.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.