Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

.
FB_IMG_1555429937706.jpeg
 
Alisema hajafurahishwa kabisa na kitendo cha Sarri kumleta ‘babu’ Gonzalo Higuain kwa kuwa hajafanya lolote tangu atue hapo dirisha la Januari. Vijana wa Sarri mpaka sasa wamefunga mabao 57 Ligi Kuu msimu huu ikiwa ni mabao pungufu kwa Liverpool na Man City.
 
Achana na Liverpool na Manchester City ambao wenyewe wamejitengenezea himaya yao pale juu, wanapigana wenyewe huku kila mmoja akisubiri mwenzake ateleze. Ligi inazidi kunoga.
Ishu ni nani na nani watazifuata Liverpool na Man City kukamilisha top four? Tusubiri mwisho wa msimu.
 
Chelsea hoi zaidi
Kwenye kinyang’anyiro hicho cha top four, ni kama hawako siriazi. Kama wakishindwa tu kutinga top four na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya, ni wazi watajilaumu wenyewe.
Hii ni kutokana na uamuzi wao wenyewe walioufanya kipindi cha usajili wa dirisha dogo la Januari.
 
Kwa sasa inahaha kutinga Top Four baada ya kichapo cha mabao 2-0 walichopata kutoka kwa Liverpool Jumapili iliyopita usiku.
Hata hivyo, Chelsea mbali na kupigana top four, kuna nafasi nyingine ya kucheza Ligi ya Mabingwa na yenyewe ni kupitia mlango wa nyuma.
 
Chelsea ilimleta Darajani straika Gonzalo Higuain akitokea Inter Milan alikokua akicheza kwa mkopo akitokea Juventus ya Italia. Lengo kubwa lilikuwa ni kuongeza makali kwenye kikosi hicho lakini tangu atue klabuni hapo, ni kama anazidi kuwa butu. Hakuna lolote la maana alilolifanya
 
Chelsea ilimleta Darajani straika Gonzalo Higuain akitokea Inter Milan alikokua akicheza kwa mkopo akitokea Juventus ya Italia. Lengo kubwa lilikuwa ni kuongeza makali kwenye kikosi hicho lakini tangu atue klabuni hapo, ni kama anazidi kuwa butu. Hakuna lolote la maana alilolifanya
 
Kwenye mchezo wao dhidi ya Liverpool, baada ya Kocha Maurizio Sarri kuona mambo hayaendi alimuingiza Higuain, hata hivyo, kuanzia dakika ya 56, aliyoingia dimbani, miguu ya Muargentina huyo ni kama ilikuwa ikitetema kwani ilikataa kabisa kuinusuru Chelsea na kipigo hicho.
 
Katika mechi 24 za ligi alizoingia dimbani msimu huu, Straika huyu wa zamani wa Real Madrid, ameifungia Chelsea mabao manne tu.
Kama kuna pahala klabu hukosea ni kununua wachezaji kwa kuzingatia takwimu zinazowekwa mitandaoni. Hiki ndicho kilichowaponza Chelsea, katika harakati za kutafuta mbadala wa Diego Costa na baadae Alvaro Morata.
 
Back
Top Bottom