Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

56656351_116088886247823_7183975082604492800_n.jpg
 
Mkataba wa Hazard utafika tamati mwishoni mwa msimu ujao na kocha Maurizio Sarri ameshamwambia wazi bilionea mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kwamba itakuwa jambo gumu sana kuendelea kubaki na staa huyo kwenye kikosi chao.
 
Chelsea wao kwa upande wao wamefanya kila walichoweza kukifanya kumtaka abaki, lakini sasa mambo magumu mwaka mmoja umebaki na hakuna makubaliano yoyote. Hazard ni wa Pauni 100 milioni na Chelsea watakuwa wendawazimu kukataa kiasi kama hicho cha pesa.”
 
MANCHESTER United inateseka sana kuziba pengo la Sir Alex Ferguson kwa miaka sita sasa, wakati Arsenal wao wameonekana kuwa na kazi nyepesi tu kumtafuta mtu sasa baada ya kocha wao mkongwe Arsene Wenger alipong’atuka.
 
Man United ndani ya miaka hiyo sita imebadili makocha wanne, David Moyes amekuja, akaondoka. Louis van Gaal akatua Old Trafford, mambo yakamshinda, naye akaondoka. Kikafika kipindi cha Jose Mourinho, wengi wakiamini Man United itakuwa kwenye mikono salama tangu alipoondoka Ferguson, akachemsha akaondoka. Sasa hivi, yupo Ole Gunnar Solskjaer kijana wa Ferguson.
 
Lakini, Arsenal wao wanaonekana kufanya chaguo sahihi walipombadili kocha wao aliyedumu kwenye timu hiyo kwa miaka mingi, Mfaransa kwa kumleta Mhispaniola, Unai Emery. Wanasema hivi, data hazidanganyi unaambiwa.
 
Zimechukuliwa mechi 50 za mwanzo wa kocha Wenger kwenye kikosi cha Arsenal na idadi kama hiyo ya mechi za Emery kwenye kikosi hicho na hapo ndipo ilipoonekana kwamba mabosi wa Arsenal walituliza akili wakati wanamsaka mtu wa kuja kuvaa viatu vya kocha aliyedumu kwenye timu kwa miaka mingi na kuonekana kama vile ni timu yake binafsi.
 
Back
Top Bottom