Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SUPASTAA, Lionel Messi amewapiga mbili Manchester United Jumanne iliyopita akisaidia Barcelona kushinda 3-0 katika mechi ya marudiano hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo, kukifanya kikosi cha Nou Camp kutinga nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-0 baada ya mechi ya kwanza kushinda 1-0 uwanjani Old Trafford.
 
Mabao yake hayo mawili aliyowafunga Man United yanamfanya Messi kuwa na rekodi nzuri ya kuzifunga timu za Top Six kwenye Ligi Kuu England, lakini swali lililopo je anachuana vipi na staa mwenzake, Cristiano Ronaldo katika kuzifunga timu vigogo wa Ligi Kuu England?
 
Tottenham – Ronaldo 10, Messi 2

Kwenye historia yake, Ronaldo amekutana na Tottenham Hotspur mara 15 katika michuano tofauti na kufunga mabao 10, wakati Messi naye amewakabili Spurs katika idadi kama hiyo ya mechi, lakini amewafunga mara mbili tu. Katika kuwakabili wababe hao wa London, Ronaldo amewafunga mara nyingi kuliko staa huyo wa Argentina.
 
Man United – Ronaldo 3, Messi 4

Staa wa Kireno, Ronaldo aliwahi kuichezea Manchester United kabla ya kwenda zake Real Madrid na sasa kukipiga huko Juventus. Tangu Ronaldo alipoondoka Man United amecheza dhidi ya timu hiyo mara nne na kufunga mabao matatu, wakati Messi kwa upande wake amekabiliana na Man United mara sita na kufunga mabao manne, mawili akifunga katika fainali mbili alizokutana na timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya Rome na London.
 
Man City – Ronaldo 5,

Messi 6

Mambo ni moto. Manchester City inakumbukumbu nzuri tu ya kumenyana na wakali hao wawili bora kabisa kwenye soka la Ulaya. Wababe hao wa Etihad wamemkabili Messi mara sita na wamefungwa mabao sita ikiwa ni wastani wa bao moja kwenye kila mechi, wakati supastaa Ronaldo alikabiliana na Man City mara 12 katika michuano tofauti na kufunga mabao matano.
 
Liverpool – Ronaldo 3, Messi 0

Liverpool watakuwa wanacheka kwa kuwa na rekodi nzuri dhidi ya supastaa wa Barcelona, Messi ambapo katika mechi mbili walizokabiliana naye, hajafunga bao lolote. Pengine safari hii wakienda kumenyana naye kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wataomba rekodi hiyo iendelee.
 
Kwa sasa kocha na mastaa wa Liverpool wanasaka mbinu za kuhakikisha Messi hatembei wala hafungi kwenye watakapokutana kwenye mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati huko kwa Ronaldo amewakabili Liverpool mara 12 katika michuano tofauti na kuwafunga mabao matatu.
 
Katika mechi 10 alizowakabili The Blues, Messi amefunga mara tatu, wakati mpinzani wake Ronaldo amecheza mechi 12 dhidi ya Chelsea na kufunga bao moja tu. Kwenye kuwakabili Chelsea, Messi ameonyesha kuwa na uwezo mkubwa kuliko Ronaldo kwa sababu amekutana nao mara nyingi kuliko Messi, lakini amefunga mara chache ukilinganisha na mpinzani wake huyo kwenye soka la dunia.
 
Arsenal – Ronaldo 6, Messi 9

Kama kuna timu iliyowahi kukutana na mateso mengi kutoka kwa Messi katika orodha ya zile zilizopo kwenye Top Six ya Ligi Kuu England basi ni Arsenal.
 
Wakali hao wa Emirates wamekabiliana na Messi mara 15 na katika mechi hizo amewafunga mara tisa, ikiwamo yale mabao yake manne aliyofunga kwenye mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Huko kwa Ronaldo kwa upande wake amecheza dhidi ya Arsenal mara 15, lakini amefanikiwa kuwafunga mara sita tu.
 
Wakali hao wa Emirates wamekabiliana na Messi mara 15 na katika mechi hizo amewafunga mara tisa, ikiwamo yale mabao yake manne aliyofunga kwenye mechi moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Huko kwa Ronaldo kwa upande wake amecheza dhidi ya Arsenal mara 15, lakini amefanikiwa kuwafunga mara sita tu.
 
Back
Top Bottom