Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amedai wachezaji wa Manchester City wanacheza ragu nyingi sana wanapokuwa hawana mpira kitu kilichofanya kuibuka kwa mjadala wa kutaka kufahamu ni timu iliyopiga rafu nyingi kwenye Ligi Kuu England msimu huu.
 
Man City – rafu 291, kadi 39

Virana wa Ligi Kuu England, Manchester City kwa rekodi za msimu huu ndio timu iliyocheza faulo chache, lakini nyingi zikidaiwa za kiufundi zaidi. Katika faulo 291 walizocheza, Man City imejikuta mastaa wake wakionyeshwa kadi 39, ambapo za njano 38 na nyekundu moja huku Fernandinho akiongoza kwa kucheza rafu.
 
Liverpool – rafu 303, kadi 38

Liverpool wamepania kwelikweli kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu wachezaji wake wakifanya kila wanachoweza kufanikisha hilo baada ya kucheza rafu 303 na kuonyeshwa kadi 38, ambapo nyekundu ni mbili na 36 ni kazi za njano, huku staa wao James Milner akiongoza kwa kucheza faulo.
 
Chelsea – rafu 311, kadi 40

Hadi sasa Chelsea haijaonyeshwa kadi yoyote nyekundu kwenye Ligi Kuu England licha ya kucheza rafu 311, huku beki wake wa kati, Antonio Rudiger akiongoza kwa kucheza mchezo mchafu uwanjani. Wababe hao wa Stamford Bridge wameonyeshwa kadi za njano 40 wakionekana kucheza kistaarabu zaidi.
 
West Ham – rafu 311, kadi 57

Kwenye Ligi Kuu England msimu huu, West Ham wamelingana na Chelsea kwa kucheza rafu wakifanya hivyo mara 311 na kuonyeshwa kadi 57, moja ikiwa nyekundu na nyingine zilizobaki ni za njano. Staa wao, Robert Snodgrass, ndiye anayeongoza kwa mchezo mchafu kwenye kikosi hicho kwa kucheza rafu nyingi.
 
Bournemouth– rafu 312, kadi 59

Kuna mchezaji mmoja tu kwenye Ligi Kuu England, ambaye ameonyeshwa kadi nyingi za njano kuliko Jefferson Lerma wa Bournemouth, akiwa ameonyeshwa kadi hizo mara 11. Bournemouth imecheza rafu 312 msimu huu na kuonyeshwa kadi mara 59, nyekundu moja na nyingine ni za njano huku Lerma akiongoza.
 
Leicester City– rafu 324, kadi 60

Kwenye Ligi Kuu msimu huu, hakuna timu iliyoonyeshwa kadi yekundu nyingi kuliko Leicester City baada ya kuonyeshwa mara tano. Wababe hao wamecheza rafu 324 na kuonyeshwa kadi 60, ambapo ukiweka kando hizo tano nyekundu zilizobaki ni za njano, huku Wilfred Ndidi akiongoza kwa mchezo mchafu.
 
Tottenham– rafu 351, kadi 52

Tottenham Hotspur imekuwa kwenye vita kali kuhakikisha inamaliza msimu ndani ya Top Four na ndio maana mastaa wake wanafanya kila wanachoweza, ikiwa pamoja na kucheza rafu 351 kwenye ligi. Spurs wameonyeshwa kadi 52, nyekundu ikiwa moja na nyingine zilizobaki ni za njano huku Harry Kane akiongoza.
 
Crystal Palace– rafu 355, kadi 55

Crystal Palace wamesifika kwa kuwa na beki imara huku wakizitesa timu pinzani kwa staili yao ya kushambulia kwa kushtukiza. Kwenye ligi, Palace amecheza rafu 355 na kuonyeshwa kadi 55, ambapo nyekundu ni mbili na zilizobaki ni kadi za njano, huku staa wao Luka Milivojevic akitajwa kuwa mchafu zaidi uwanjani.
 
Cardiff City– rafu 346, kadi 64

Kikosi cha Neil Warnock kinapambana na hali yake kuhakikisha kinaendelea kubaki kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Cardiff City msimu huu wamecheza rafu 346 na kuonyeshwa kadi 64, nyekundi moja na nyingine ni kadi za njano huku staa wao Sol Bamba akiongoza kwa kucheza soka chafu ndani ya uwanja.
 
Burnley – rafu 335, kadi 68

Straika wa Burnley, Ashley Barnes ameripotiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaoongoza kwa kupiga rafu kwenye kikosi hicho, huku timu nzima ikipiga rafu 335 na kuonyeshwa kadi 68, ambapo kadi za njano ni 67 na moja tu ndio nyekundu. Kadi 67 za njano zimewafanya Burnley kushika namba tatu msimu huu.
 
Wolves – rafu 365, kadi 66

Kiboko ya vigogo wa Top Six kwenye Ligi Kuu England, Wolves wamecheza soka la kibishi msimu huu wakicheza rafu 365 na kuonyeshwa kadi 66, ambapo nyekundu ni moja na nyingine zilizobaki ni kadi za njano. Beki wao, Ryan Bennett ndiye aliyetajwa kucheza rafu nyingi zaidi kwenye kikosi hicho kuliko wengine wote.
 
Newcastle United– rafu 395, kadi 55

Kikosi cha Rafa Benitez kinacheza bila ya presha ya kushuka daraja. Hata hivyo kufanya hivyo wamepambana kwelikweli ikiwamo kuwapiga rafu wapinzani mara 395 na kuonyeshwa kadi 55, ambapo mbili ni nyekundu na nyingine zilizobaki ni za njano, huku staa wao Matt Ritchie akiongoza kwa mchezo mchafu uwanjani.
 
Arsenal – rafu 378, kadi 63

Granit Xhaka ndiye anayeongoza kwa rafu kwenye kikosi cha Arsenal msimu huu, ambapo kwa ujumla wake kikosi hicho cha kocha Unai Emery kimepiga rafu 378 na kuonyeshwa kadi 63, huku nyekundu ikiwa ni moja tu na nyingine ni kadi za njano. Kadi nyekundu alionyeshwa Lucas Torreira dhidi ya Tottenham.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…