Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

South Africa,
Hakujapoa
FB_IMG_1556435393101.jpeg
 
Hata hivyo, bado kocha wa timu hiyo, Pepp Guardiola hajaamua hasa kama kweli anaitaka huduma ya Messi.

Lakini kuna ambao waliupiga mpira mwingi. Na wenyewe wapo wa kutosha lakini hawakuwahi kuigusa EPL hadi walipoamua kutundika daruga kwamba ama walicheza ligi nyingi au walimaliza kwenye ligi moja.
 
Mastaa kadhaa walivuma duniani lakini ama walicheza Ligi ya Hispania au Italia na kwa kiasi fulani walicheza Ujerumani.

Wafuatao ni baadhi ya mastaa saba waliotikisa dunia kwa soka ambao pia baadhi yao walikuwa kwenye rada za klabu za EPL na kama mambo yangeenda sawa basi wangecheza EPL lakini hadi wanastaafu, hakuna.
 
KAKA

Ricardo Izecson dos Santos Leite, maarufu kama Kaka ni mmoja kati ya wachezaji waliokua kipenzi cha Wabrazil na nimchezaji wa mwisho wa Kibrazil kushinda tuzo ya Ballon d’Or.

Kaka alianza maisha yake ya soka Sao Paolo kabla ya msimu wa 2003/04, kujiunga na AC Milan. Alicheza soka la kulipwa Italia kwa miaka sita ambapo alifunga mabao 95 kwenye michezo 270.
 
2009 Real Madrid ilipata saini yake lakini hakuwa na maisha mazuri ndani ya klabu hiyo kutokana na kusumbuliwa kwake na majeraha ya mara kwa mara.

Kaka alirejea Milan na mwishowe akaenda kumalizia soka Marekani kwenye klabu ya Orlando City MLS hadi anastaafu soka mwaka jana, Kaka hakuwahi kucheza soka nchini England licha ya kipindi alichokuwa kwenye ubora wake kuhusishwa kujiunga na Manchester City.
 
PAVEL NEDVED

Gwiji wa Jamhuri ya Czech, Pavel Nedved vijana wa kiasasa tungeweza kumwita alikuwa ‘mido kisheti’ kutokana na uwezo wake wa kumudu vyema kucheza kwenye eneo la kiungo.

Nedved alikuwa sehemu ya kikosi cha Czech kilichotinga Fainali za Euro 1996. Kiungo huyo ana tuzo mkononi mwake ya Ballon d’Or aliyotwaa 2003 kabla ya kwenda kushinda tuzo nyingine kubwa ya mchezaji bora wa mwaka Ulaya.
 
Nedved alianza kucheza soka kwenye klabu ya Dukla Prague msimu wa 1991/92, kabla ya msimu uliofuata kuhamia Sparta Prague. Msimu wa 1995/96, Nedved alifunga mabao 19 kwenye michezo 38 kitu kilichowastua miamba ya soka ya Italia,Lazio kuamua kumsajili.

Alifanya vizuri Lazio ambako alishinda mataji kadhaa na mwishowe Juventus ikamsajili kama mbadala wa Zinedine Zidane na kucheza kwa mafanikio makubwa ndani ya miaka yake nane akiwa Turin hadi msimu wa 2008/09 alipotangaza kusaafu soka.
 
ANDREA PIRLO

Andrea Pirlo ni miongoni mwa viungo bora kuwahi kutokea kwenye uso wa dunia. Alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa la Italia kilichochukua ubingwa wa kombe la dunia 2006 kwenye ardhi ya Ujerumani.

Alianza kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Brescia ambako alishinda huko taji la Serie B . Alihama kwenda Inter Milan, aliposhindwa kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza alirejeshwa kwenye timu yake ya zamani kwa mkopo.
 
Mismu wa 2001/02, Pirlo alijiunga na AC Milan. Aliichezea timu hiyo kwa msimu 10 ambayo alishinda Serie A mara mbili, Ligi ya Mabingwa Ulaya na UEFA Super Cups mara mbili, FIFA Club World Club, Supercoppa Italiana na Coppa Italia.

Pirlo alijiunga na Juventus, 2011 kama mchezaji huru na akafanikiwa kushinda mataji manne ya Serie A, Turin tena akashinda Coppa Italia na Supercoppa Italiana mara mbili baada ya mkataba wake kumalizika alienda zake Marekani.
 
Back
Top Bottom