Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HABARI ndiyo hiyo. Ule utamu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya umerudi wiki hii, leo Jumanne kitapigwa kipute cha kwanza cha nusu fainali huko London, wakati Tottenham Hotspur itakapoikaribisha Ajax, wakati shughuli pevu zaidi itakuwa kesho Jumatano huko Nou Camp, Liverpool watakapokwenda kumkabili Lionel Messi.
 
Macho ya wengi yatasubiri kuona kama ngome ya Barcelona itakuwa kwenye mateso makubwa itakapokutana na fowadi ya wakali watatu moto kabisa wa huko Anfield, Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino wakati watakapokwenda kufanya yao huko Nou Camp.
 
Mechi hiyo itawakutanisha Liverpool na wakali wao wa zamani Suarez na Coutinho na hicho ndicho kinachowafanya kuwapo kwa mvuto mkubwa kwenye mechi hiyo ambapo Barcelona wao watakuwa hawana presha yoyote kwa maana tayari wameshajibebea taji la La Liga.
 
Kikosi cha kocha Mauricio Pochettino kina mastaa kibao waliotoka Ajax, lakini hakuna ubishi wababe hao wa Uholanzi kwa sasa ndiyo wenye wachezaji walio kwenye viwango bora kabisa kiasi cha kuwafanya vigogo kibao kuwapigia hesabu kuwasajili.
 
Nusu fainali hizo za kwanza zitapigwa wiki hii, wakati mechi za marudiano zitakuwa wiki ijayo, ambapo mwenye ushindi mzuri ndiye atakayefika fainali, huku Liverpool wao wakisaka fainali yao ya pili mfululizo baada ya msimu uliopita kufika hatua hiyo na kuchapwa na Real Madrid.
 
Hakikuwa kitu cha kushangaza kuona Manchester City na Liverpool zikiongoza kwa kuwa na wachezaji wengi, huku timu nyingine moja iliyofanikiwa kuingiza mchezaji wake ni Manchester United, Paul Pogba.
 
6. Arsenal - 8

Licha ya kwamba Arsenal hawajabeba ubingwa wa Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 11 sasa, lakini bado wachezaji wake mmoja mmoja wamekuwa wakitamba na hivyo kupata nafasi ya kuwamo kwenye vikosi bora vya msimu kwenye Ligi Kuu England.
 
Kwa kuanzia mwaka 2008, Arsenal imeingiza wachezaji wanane kwenye vikosi bora vya msimu na katika msimu wa 2010/11 iliingiza wachezaji watatu, Bacary Sagna, Jack Wilshere na Samir Nasri. Msimu huu ikiwa chini ya kocha Unai Emery imeshindwa kuingiza mchezaji huku staa wao wa mwisho kuwamo kwenye kikosi hicho alikuwa Hector Bellerin misimu mitatu iliyopita.
 
5. Liver– wachezaji 13

Liverpool kwenye kiwango bora msimu huu na kimengiza wachezaji wengi kikosi bora cha msimu ikiingiza wachezaji wanne. Kwa ujumla wake, Liverpool imewahi kuingiza wachezaji 13 kwenye vikosi bora vya msimu. Misimu ya hivi karibuni wanatesa baada ya kocha Jurgen Klopp kutengeneza timu ya kiushindani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…