Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

lakini ghafla tu mambo yamebadilika na kiungo huyo amekuwa akicheza chini ya kiwango siku za karibuni jambo linalodaiwa kwamba huenda anataka kuondoka baada ya kukiri kwamba anatamani kwenda kucheza Madrid chini ya Zidane.
 
Staa mwingine wa kiwango cha dunia anayesakwa na timu hiyo ni Eden Hazard wa Chelsea ambapo kocha Zidane ameripotiwa kuwa na mkwanja mrefu wa kunasa vichwa vya maana tupu anavyotaka kwenye kikosi chake.
 
Liverpool imepata pigo kubwa baada ya staa wake Mohamed Salah kupata majeruhi ya kichwa jambo lililomfanya aangue kilio wakati alipokuwa akitolewa uwanjani kwa machela kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United Jumamosi huko St James' Park.
 
Fowadi huyo wa kimataifa wa Misri aligongana na kipa wa Newcastle, Martin Dubravka katika kipindi cha pili kwenye mchezo ambao Liverpool walirejea kileleni kwenye msimamo wa ligi baada ya kushinda 3-2 ugenini.
 
Majeruhi hayo yanamweka kwenye mashaka makubwa ya kuwakabili Barcelona kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne huko Anfield, lakini akiwa kwenye hofu kubwa pia ya kukosa mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England dhidi ya Wolves Jumapili.
 
Unajua Mkuu Damushin watu wengi hawapendi ukweli ndiyo maana Mimi baada ya kushahuri sikutumia nguvu nyingi kuwalazimisha ukweli huwezi ukawa unajua kabisa huna uwezo wa ku Afford kwenda Disney land kula bata na bado ukajipa moyo inawezekana

Ni sawa kwa Mzee wa liver kuamini watapindua matokeo na kuwaondoa Mashindanoni Barcelona
Hahahahaha mkuu
 
Back
Top Bottom