Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aidha, Hifadhi ya Jamii husaidia Wafanyakazi katika sekta ya Umma na Binafsi kukabiliana na gharama matibabu na matatizo mengine ya kijamii. Mkulima naye anaweza kupata mafao Haya ya Matibabu ( Bima ya Afya ) na hata mafao yanayohusiana na kazi zake za Kilimo kama vile Fao la Bei na hata Bima ya Mazao. Kiufupi Hifadhi ya Jamii ni mfumo wa Akiba ya lazima ya muda mrefu yenye kuendana na faida za muda mfupi. Pia ni mfumo wa Uwekezaji wa Muda mrefu ili kukabiliana na majanga ya muda wote.
 
Kwa sekta ya Kilimo mfumo huu unaweza kufanya kazi kwa kuweka mfumo wa akiba kupitia vyama vya ushirika vya Wakulima na pia Serikali kutenga sehemu fulani ya Bajeti kuchangia Katika Skimu. Kwa mfano kwenye mazao ya Biashara ushuru maalumu utawekwa kuchangia Katika Skimu.
 
Mfano Ushuru wa Korosho ( exports levy) ungeweza kutumika kwa Wakulima wa Korosho badala ya Serikali kuziweka Fedha hizi kwenye matumizi yake. Ushuru kama huu ungewekwa kwenye mazao mengine ya Biashara kama
Vile Kahawa, Pamba nk. Mikopo nafuu kwa Wakulima na mafao mengine ya muda mfupi yanaweza kutolewa kupitia Vyama vya Wakulima wa mazao husika. Uwekezaji wa Skimu pia ungefanywa kwa ajili ya kukuza sekta na haswa kuwezesha kuongeza tija Katika Sekta.
 
Nasaha yangu kwa Serikali ni kuanzisha Skimu ya Hifadhi ya Jamii ya Wakulima ili kuwavutia kuweka akiba, kupata bima ya afya, Fao la Bei na mikopo nafuu ya pembejeo.

Fao la Bei husaidia bei ya mazao ikianza kushuka. Kwa sasa Bei za mazao zikishuka Wakulima watarudi kwenye umasikini kwani hawana fidia ya Bei kushuka ( Fao la Bei). Kukiwa na PRICE STABILISATION Mkulima anakuwa na hakika hata bei ikishuka chini ya kiwango Cha gharama zake za uzalishaji Skimu ya Hifadhi ya Jamii itamfidia na hivyo kuendelea na shughuli zake msimu unaofuata.
 
Sharia ya makosa ya kujamiiana zinampendelea zaidi mwanamke na kukiuka haki za mwanaume, sheria hizo zimemchukulia mwanaume kuwa mtu katili bila kujali umri wake
 
Ina lillah waina ilahyi rajuun
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…