Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

United ilifikia katika Hoteli ya Meliá Gran iliyopo kilomita 32 kutoka Pwani ya Barcelona. Mastaa wawili wa United, Nahodha Roy Keane na kiungo, Paul Scholes walikuwa wamesimamishwa baada ya wote kupewa kadi za njano za pili katika pambano la nusu fainali dhidi ya Juventus.
 
Kocha wa United, Sir Alex Ferguson awali alifikiria kumchagua winga Ryan Giggs kucheza na Nicky Butt katikati ya uwanja lakini baadaye akaamua kumchezesha David Beckham eneo la katikati. Upande wa kulia akampanga Giggs wakati kushoto akampanga winga wa kimataifa wa Sweden, Jesper Blomqvist.
 
Katika pambano hilo, mchezaji mwingine aliyekosa nafasi ni beki wa Norway Henning Berg ambaye alikuwa majeruhi na hii ilimaanisha staa mwenzake wa Norway, Ronny Johnsen ambaye awali ilidhaniwa angecheza na Butt katikati alilazimika kuanza katika ukuta na mbabe, Jaap Stam.
 
Huku Keane akishindwa kucheza pambano hilo, golikipa, Peter Schmeichel ambaye Novemba 1998 alitangaza angeachana na United mwishoni mwa msimu, alipewa kitambaa cha unahodha katika mechi hiyo na hii ilimaanisha makipa wote wawili, Schmeichel kwa United na Oliver Kahn kwa Bayern wangekuwa manahodha wa mechi hiyo.
 
Wafungaji bora wa United msimu huo, Andy Cole na Dwight Yorke walianza mbele huku Teddy Sheringham aliyecheza vema mechi ya fainali za FA siku chache zilizopita akianzia benchi. Wengine katika benchi la United walikuwa ni Ole Gunnar Solskjær, kipa Raimond van der Gouw, mabeki David May, Phil Neville na Wes Brown, pamoja na kiungo Jonathan Greening.
 
Back
Top Bottom