Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kukosekana kwa Elber kulisababisha Bayern ichezeshe washambuliaji watatu mbele, Mario Basler, Carsten Jancker na Alexander Zickler. Nafasi ya Lizarazu ikachezwa na Michael Tarnat huku Markus Babbel akicheza kulia.
 
IMG-20190528-WA0016.jpeg
 
Babbel alichezeshwa kwa ajili ya uwezo wake wa kukaba zaidi na kocha akamuacha benchi Thomas Strunz ambaye anajulikana kwa kushambulia zaidi. Hata hivyo, maamuzi ya Ferguson kumpanga Gigs kulia yalisababisha Giggs akutane na Tarnat na sio Babbel.
 
Ukuta wa Bayern uliongoza na Lother Matthaus (Kiungo Mkabaji), Thomas Linke na Mghana, Samuel Kuffour ambaye alikuwa mchezaji pekee asiye wa Kijerumani katika kikosi cha Bayern huku United ikiwa na wachezaji wanne tu wa Kiingereza kikosini.
 
Kipindi cha kwanza

Mpira ulipoanza, ndani ya dakika sita za kwanza, Johnsen alimchezea madhambi Carsten Jancker nje kidogo ya boksi la United na Mario Basler akafunga mpira wa faulo vema. Alidanganya kama anapiga juu ya ukuta lakini waliporuka akapiga katika nyayo zao.
 
Pamoja na kuanza ovyo lakini United ikajitahidi kumiliki mpira huku David Beckham akikimbia bila ya kuchoka. Walionekana wanawakosa viungo wao mahiri Paul Scholes na Roy Keane. Ukuta wa Bayern ulionekana kuwa imara na umejipanga.
 
Back
Top Bottom