Kuna watu wanatumia neno uzalendo kama pazia la kuficha ‘ujinga’ uliojaa kwenye kauli zao; kwamba ukiongea pumba halafu ukasingizia uzalendo basi watu wenye uelewa mdogo wa mambo watakuona unaingea ‘pointi’ za msingi. Ni bahati mbaya kwamba,
Mtu anayesema Tanzania haitapiga goti kuomba misaada, ndiye huyo aliyetumwa kwenda kulialia mbele ya wakuu wa nchi za Ulaya ili Tanzania isiwekewe vikwazo – na kukubali masharti. Kwa bahati mbaya, mtu anayesema Tanzania haitapiga goti kuomba msaada hana uwezo, na hakuwahi kuonesha hata dalili ya kuwa na uwezo wa kuisaidia Tanzania iondokane na misaada.