Wachungaji wa aina hii hawawezi kuongelea mafanikio ya watu weusi kama Barack Obama, Serena Williums, na Usain Bolt. Hawawezi kuongelea wagunduzi waliosaidia kutransform dunia kama kina Albert Einstein, Steve Jobs na wengine. Hawawezi kuongelea Wanasayansi waliodedicate maisha yao na wengine kufia maabara wakitafuta dawa za kutibu magonjwa mbalimbali yanayoisumbua Afrika.
Hawawezi kuongea kuhusu wanafasihi vijana kama Chimamanda Ngozi na Ben Okri, au wanafasihi wakongwe kama Chinua Achebe na Ngugi wa Thiong'o.
Kila pembe ya dunia kuna watu waliofanikiwa kutokana na maarifa, bidii, ubunifu, na weledi. Wapo wafanyabiashara, wanasiasa, wanafasihi na hata wanasayansi wanaofanya mambo makubwa ya kuisaidia dunia yetu. Lakini wachungaji wa Afrika hawatawaongelea watu wa aina hii.