moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 159,165
- 777,891
Ndiyo tulivyo hasa sisi wafrika
Hata Putin amekuwa akitukoromea sana bro...Nini mchango wako kuhusu hili bro kuna ukweli wowote kwenye huu ujumbe mchungu na mzito
Haiwezekani hii kitu.Kama nilivyobatizwa na Prisca, Mimi Ngosha The Don naileta thread hii hapa kwa faida ya mabinti maandaeitini wote walio katika uzi huu. Hata wale ambao sio maandaeitini (30+) ujumbe huu utawafaa sana. Blessings [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
![]()
Wanawake stress nyingine tunazitafuta
Mmekaa sitting room mnaangalia taarifa ya habari, simu ya mr inaita, anaamka anachukua simu, ameamua kuongelea chumbani. Baada ya maongezi anarudi anakukuta mwanamke umeumuka kama umetiwa hamira, aliyepiga simu ni nani? Kama ungetakiwa kumjua au kujua wanayoongea asingeenda chumbani, yeye ni...www.jamiiforums.com
Akhaa[emoji317][emoji317]Wewe hauko singo? [emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
Haiwezekani hii kitu.
Nafurahi umeandika ukweli MpendwaMimi sio Binti lakini nakubaliana na wewe haiwezekani unless huyo mwanamke awe na umri kuanzia 50 na mzoefu sana
Huu ni mtizamo wa Ngugi wa Thiong'o na unaungwa mkono na watu wengi (mimi nikiwemo). Ni ukweli usiopingika kuwa wamishenari wa kwanza walitumiwa vyema sana kama waandalizi wema kumuandaa Mwafrika kisaikolojia ili atawalike kirahisi...(Mamlaka yote yanatoka kwa Mungu, Ukipigwa shavu la kushoto geuza na lingine...). Wakafanikiwa sana kumwaminisha Mwafrika kuwa alikuwa ni kiumbe duni asiye na ustaarabu, kiumbe wa bara la giza asiye na mchango wo wote katika ustaarabu na maendeleo ya dunia. Ngozi nyeusi ikageuzwa nembo ya shetani na madhila yote yanayoambatana nayo. Lugha za Mwafrika zikaitwa duni zisizo na mawanda mapana ya kimawasiliano. Dini zake zikatwishwa ushetani. Utamaduni wote ukavurugwa. Dunia ikaaminishwa kuwa Mwafrika hajatoa mchango wo wote wa maana katika maendeleo ya dunia hii.
Hoja kuu ya Ngugi ni kwamba lugha na utamaduni wa mtu ndiyo humtambulisha hapa duniani yeye pamoja na nafasi yake. Yeye ni nani? Alitoka wapi? Nafasi yake ni ipi katika mifumo mbalimbali inayotawala na kuendesha dunia hii? Falsafa yake ni ipi kuhusu maisha na jukumu lake la msingi kwake yeye na vizazi vyake vijavyo kijamii, kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kimaendeleo- katika mawanda ya kwake na hata kimataifa?
Ukishamvurugia mtu utamaduni wake unakuwa umetoa roho yake ya kiutashi na kimtazamo. Anakuwa msukule. Bendera fuata upepo tu na atafanya cho chote utakachokitaka hata kama ni kibaya kwake na watu wake. Anakuwa hana misingi. Hana mifumo yake mwenyewe ya kujiendeshea maisha. Anakuwa tegemezi. Ndiyo maana wazungu na jamii nyingine zinazojitambua wako makini sana kulinda utamaduni wao na lugha zao. Waangalie Wajapani. Wachina. Wakorea. Wahindi...isipokuwa sisi.
Na ukiangalia vyema Wazungu walifanikiwa sana katika hili. Mtu mweusi yupo tu kama zombie. Hana utamaduni wake. Hana mifumo yake mwenyewe. Mtawaliwa wa kisaikolojia, kifalsafa, kiutashi na hata kiutu. Na dini ni nyenzo muhimu sana iliyofanikisha zoezi hili. Wangetaka kutafsri vitabu vingine wangeweza hasa katika mashule lakini kufanya hivyo kungemsaidia nani? Ingekuwa ni sawa na kujimaliza wao wenyewe na kwenda kinyume na lengo kuu lililokuwa limewaleta.
Kilio cha Ngugi na kundi lake ni kwa mtu mweusi kujitambua. Kurudi katika utamaduni wake. Kujaribu sana kujiundia mifumo yake mipya ya kuendeshea maisha yake. Kuiona thamani yake aliyokuwa nayo kabla hajakalishwa chini kisaikolojia. Afike mahali abadilishe mifumo hii aliyorithishwa. Mifumo ya elimu. Mifumo ya kisiasa isiyoendana na utamaduni na historia yake. Mifumo mipya ya kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo mvuvumko wa kweli utatokea kwa Afrika na pengine safari ya maana kuelekea kwenye maendeleo kikiki itaanza. Vinginevyo Afrika, pamoja na utajiri wake wote, itabakia tu ikizunguka katika mzunguko butu huu wa umasikini, siasa za hovyo, mifumo ya elimu iliyopitwa na wakati, ufisadi wa kinyama na madhila mengine lukuki....
(Nilikuwa na muda mrefu sijaandika gazeti humu. Mama Mlonge si ajabu atakuja kunigombesha [emoji16][emoji16][emoji16])
Hata Putin amekuwa akitukoromea sana bro...
View attachment 1123803
Nafurahi umeandika ukweli Mpendwa
Mnajipa steresi za bure tu..Haiwezekani hii kitu.
Tuna safari ndefu
Ukipata wa hivyo bro utakuwa na ndoa ya amani sana. Cha muhimu kuheshimiana ati !Yaliyo andikwa kwenye ile mada yanawezekana lakini kutokea kwake kunahitaji aina flani hivi ya watu, si kizazi hiki cha modern relationship sababu kila mmoja anaweza ku reason kukonekti doti
Kwa Sasa bado tuna nguvu za kudeal na tress. Cc AtotoMnajipa steresi za bure tu..