Cole Williams
JF-Expert Member
- Jun 1, 2016
- 35,345
- 201,629
5. Without a higher spiritual purpose any bond can weaken and break
Si ajabu hata hawa wanasiasa wetu ni zao la hao hao wazungu.Huu ni mtizamo wa Ngugi wa Thiong'o na unaungwa mkono na watu wengi (mimi nikiwemo). Ni ukweli usiopingika kuwa wamishenari wa kwanza walitumiwa vyema sana kama waandalizi wema kumuandaa Mwafrika kisaikolojia ili atawalike kirahisi...(Mamlaka yote yanatoka kwa Mungu, Ukipigwa shavu la kushoto geuza na lingine...). Wakafanikiwa sana kumwaminisha Mwafrika kuwa alikuwa ni kiumbe duni asiye na ustaarabu, kiumbe wa bara la giza asiye na mchango wo wote katika ustaarabu na maendeleo ya dunia. Ngozi nyeusi ikageuzwa nembo ya shetani na madhila yote yanayoambatana nayo. Lugha za Mwafrika zikaitwa duni zisizo na mawanda mapana ya kimawasiliano. Dini zake zikatwishwa ushetani. Utamaduni wote ukavurugwa. Dunia ikaaminishwa kuwa Mwafrika hajatoa mchango wo wote wa maana katika maendeleo ya dunia hii.
Hoja kuu ya Ngugi ni kwamba lugha na utamaduni wa mtu ndiyo humtambulisha hapa duniani yeye pamoja na nafasi yake. Yeye ni nani? Alitoka wapi? Nafasi yake ni ipi katika mifumo mbalimbali inayotawala na kuendesha dunia hii? Falsafa yake ni ipi kuhusu maisha na jukumu lake la msingi kwake yeye na vizazi vyake vijavyo kijamii, kiuchumi, kisiasa, kitamaduni, kimaendeleo- katika mawanda ya kwake na hata kimataifa?
Ukishamvurugia mtu utamaduni wake unakuwa umetoa roho yake ya kiutashi na kimtazamo. Anakuwa msukule. Bendera fuata upepo tu na atafanya cho chote utakachokitaka hata kama ni kibaya kwake na watu wake. Anakuwa hana misingi. Hana mifumo yake mwenyewe ya kujiendeshea maisha. Anakuwa tegemezi. Ndiyo maana wazungu na jamii nyingine zinazojitambua wako makini sana kulinda utamaduni wao na lugha zao. Waangalie Wajapani. Wachina. Wakorea. Wahindi...isipokuwa sisi.
Na ukiangalia vyema Wazungu walifanikiwa sana katika hili. Mtu mweusi yupo tu kama zombie. Hana utamaduni wake. Hana mifumo yake mwenyewe. Mtawaliwa wa kisaikolojia, kifalsafa, kiutashi na hata kiutu. Na dini ni nyenzo muhimu sana iliyofanikisha zoezi hili. Wangetaka kutafsri vitabu vingine wangeweza hasa katika mashule lakini kufanya hivyo kungemsaidia nani? Ingekuwa ni sawa na kujimaliza wao wenyewe na kwenda kinyume na lengo kuu lililokuwa limewaleta.
Kilio cha Ngugi na kundi lake ni kwa mtu mweusi kujitambua. Kurudi katika utamaduni wake. Kujaribu sana kujiundia mifumo yake mipya ya kuendeshea maisha yake. Kuiona thamani yake aliyokuwa nayo kabla hajakalishwa chini kisaikolojia. Afike mahali abadilishe mifumo hii aliyorithishwa. Mifumo ya elimu. Mifumo ya kisiasa isiyoendana na utamaduni na historia yake. Mifumo mipya ya kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia. Ni kwa kufanya hivyo tu ndiyo mvuvumko wa kweli utatokea kwa Afrika na pengine safari ya maana kuelekea kwenye maendeleo kikiki itaanza. Vinginevyo Afrika, pamoja na utajiri wake wote, itabakia tu ikizunguka katika mzunguko butu huu wa umasikini, siasa za hovyo, mifumo ya elimu iliyopitwa na wakati, ufisadi wa kinyama na madhila mengine lukuki....
(Nilikuwa na muda mrefu sijaandika gazeti humu. Mama Mlonge si ajabu atakuja kunigombesha [emoji16][emoji16][emoji16])
Tuseme ukweli mkuu ndoa ikifika hatua hiyo ina heshima kweli.Mfano kwako mkeo anapigiwa simu anaenda kuongelea mbali nawe hiyo ni Ndoa ya heshima kweli.Ukipata wa hivyo bro utakuwa na ndoa ya amani sana. Cha muhimu kuheshimiana ati !
Anatakiwa aipokee kwanza halafu anaomba samahani, vivyo hivyo na mwanaume pia.Tuseme ukweli mkuu ndoa ikifika hatua hiyo ina heshima kweli.Mfano kwako mkeo anapigiwa simu anaenda kuongelea mbali nawe hiyo ni Ndoa ya heshima kweli.
Tatizo ni kuongea mbali na simu hii kitu mimi siwezi kuvumilia nijue tu ukweli kina zungumzwa kitu gani 😀😀😀Anatakiwa aipokee kwanza halafu anaomba samahani, vivyo hivyo na mwanaume pia.
Ni zao la mifumo ile ile ya elimu, kijamii, kisiasa na mingineyo. Ndo maana hata wakija wapya mambo ni yale yale. Karibu bara zima liko pale pale linapiga makitaimu ya kufa mtu japo tunabadili viongozi kila kukicha. Maneno matamu na kujipiga kifua sana wakiwa nje lakini wakiingia ulingoni mambo ni yale yale...wanaishia kufumwa mumo kwa mumo na utando sugu wa mifumo kengeufu tuliyoachiwa...Si ajabu hata hawa wanasiasa wetu ni zao la hao hao wazungu.
Kama namuamini mke wangu na ameniomba excuse kuwa hiyo ni private call wala sitakuwa na wasiwasi...Tuseme ukweli mkuu ndoa ikifika hatua hiyo ina heshima kweli.Mfano kwako mkeo anapigiwa simu anaenda kuongelea mbali nawe hiyo ni Ndoa ya heshima kweli.
Kama ni hivyo ubarikiwe kwenye ndoa yako mpendwaKama namuamini mke wangu na ameniomba excuse kuwa hiyo ni private call wala sitakuwa na wasiwasi...
We acha tu huyu Moudy atanifanya nihame huu uzi...Mambo ya kuota usiku mijoka ya nini
Mchana wanaweka picha za mijoka inayo tisha usiku chui, simba yaani 🤔We acha tu huyu Moudy atanifanya nihame huu uzi...Mambo ya kuota usiku mijoka ya nini
Moudgulf na Mzee wa liver. Punguzeni picha za majoka. Wenye phobia za ukweli wanateseka mpaka wanatishia kuhama uzi jamani uwii mane lavusi mi indeed wallahi !!!. Afadhali muweke picha za mende na tandu tutavumilia [emoji16][emoji16][emoji16]Mchana wanaweka picha za mijoka inayo tisha usiku chui, simba yaani [emoji848]