Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uwezekano wa Pogba kukipiga Madrid umezidi kuonekana kutokana na kudorora kwa uhusiano na kocha wake wa sasa, Ole Gunnar Solskjaer baada ya awali kutokuwa na uhusiano mzuri na kocha aliyepita, Jose Mourinho.
 
Pogba pia alikwaruzana na mashabiki wa United katika pambano la mwisho la msimu dhidi ya Cardiff City Old Trafford baada ya United kuchapwa mabao 2-0 na mashabiki walimwambia Kocha Solskjaer amuuze kama kuna uwezekano huo.
 
Mapema wiki iliyopita, mmoja kati ya waandishi wakongwe wa soka la Hispania, Eduardo Inda alikiambia kituo kimoja cha televisheni nchini humo kuwa Madrid inatazamiwa kumfuata Pogba baada ya kumalizana na Hazard huku akitoboa siri kuwa Pogba amekubali kukatwa mshahara wake ili kukamilisha dili hilo.
 
Dili la Pogba ni kama vile limekamilika. Wa kwanza kununuliwa atakuwa Hazard kisha Pogba. Amekubali kukatwa mshahara kutoka aliokuwa analipwa na Manchester United Pauni 13 milioni kwa mwaka hadi Pauni 10 milioni,” alisema Inda.
 
Adidas wanalazimisha sana aende kwa sababu ni mmoja kati ya wachezaji wao wakubwa ambao wanawatangazia bidhaa zao. Nadhani dau lake la kumnunua linaweza kuwa Pauni 137 milioni hadi 150 milioni,” aliongeza Inda.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]
1560172757188.jpeg
 
Back
Top Bottom