Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Njia za kuweka na kutoa pesa

Zama zimebadilika, maisha ya kwenda kuunga foleni benki siku nzima ili kutoa au kuweka pesa yamepitwa na wakati. Benki nzuri na za kisasa zinatoa huduma mbalimbali kama vile kutoa au kuweka pesa kwa kupitia mawakala au simu za mkononi.

Ni muhimu ukachunguza kama benki unayotaka kuichagua ina huduma hizo na ni za uhakika.
 
Kuenea kwa benki

Kuna benki zina tawi moja au mawili nchi nzima. Kujiunga na benki kama hii kunaweza kukusababishia changamoto nyingi.

Hakikisha benki unayoichagua imeenea kwa kiwango cha kutosha hata ikibidi nje ya nchi ili usikose huduma za kifedha mara uwapo mahali popote.
 
[emoji23][emoji23]
FB_IMG_1564470081904.jpeg
 
Benki katika mtandao

Kama nilivyotangulia kusema, mambo yamebadilika; hivi leo pesa hazitumiki katika masoko au maduka ya kawaida pekee.

Unaweza kutuma na kupokea pesa kwenye mtandao wa intaneti, unaweza kununua na kuuza vitu kwenye intaneti au hata kuingia kwenye akaunti yako ya benki kwa kupitia mtandao.

Kwa kufahamu hili, ni muhimu kuhakikisha kama benki unayotaka kuichagua ina huduma za kibenki za kwenye mtandao ili usikwame mahali.
 
Huduma kwa wateja

Huduma nzuri na ya uhakika kwa wateja ni kiashiria kikubwa cha biashara au taasisi bora. Unapotumia benki unaweza kukutana na changamoto kadhaa au ukahitaji kufahamu mambo kadhaa.

Ni muhimu kuhakikisha huduma kwa wateja katika benki unayotaka kuichagua ni ya uhakika.
 
Huduma zinazopatikana

Kila benki ina huduma zake au kwa lugha nyingine bidhaa zake inazotoa kwa wateja. Ni muhimu ukachagua benki ambayo ina huduma au bidhaa unazozihitaji na zenye manufaa kwako.

Chunguza maswala kama vile mikopo, bima, aina za akaunti, n.k. ili kuona kama zinakufaa na kukidhi mahitaji yako.
 
Back
Top Bottom