Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Eti kwa uhamisho wa Pauni 30 milioni, beki huyo wa zamani wa Man United, alivimba huko mitaani kwa miaka mingi tu. Wala sishangazwi na tambo za Rio.
Miaka hiyo ilikuwa ni nadra sana kusikia klabu imetumia pesa nyingi kusajili beki. Hata hivyo, kwa sasa mambo yamebadilika sana.
 
10. JOHN STONES
Beki wa zamani wa Everton, John Stones, alifuatiliwa na Guardiola kwa muda mrefu, kabla ya kukubali kutua Etihad mwaka 2016 kwa dau la uhamisho la Euro 55.6 milioni.
Fedha hizi hazikuenda bure, tangu ajiunge na Manchester City, Stones amekuwa nguzo imara kwenye ngome ya ulinzi akicheza sambamba na mwanaume, Vincent Kompany.
 
Ungeongezea na cheche ungepata zote. Kwa sasa nakupa 39/40 [emoji122][emoji122][emoji122]
 
9. DAVID LUIZ
Huyu ndiye aliyevunjilia mbali majigambo ya Rio Ferdinand. David Luiz, alisajiliwa na PSG mwaka 2014 kwa dau la Euro 56 milioni, akaweka rekodi mpya ya dunia (wakati huo).
Usajili huu ndio uliobadili upepo kwenye soko la uhamisho. Ni kuanzia mwaka huu, ambapo mabeki walianza kuwa ghali huko sokoni. Kila klabu iliamua kupandisha bei za bidhaa. Ukawa ndio utaratibu!
 
8. AARON WAN-BISSAKA
Mchezaji kinda wa Uingereza, Aaron Wan-Bissaka, anayecheza katika nafasi ya beki ya kulia ni mmoja wa sajili mpya zilizofanywa na Ole Gunnar Solskjaer katika majira haya ya usajili.
Muingereza huyu aliigharimu Manchester United kiasi cha Euro 56 milioni kutoka Crystal Palace kwenda Old Trafford. Usajili huu ulikamilishwa mara tu baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.
Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, ambaye ni mchezaji muhimu katika kikosi cha timu ya England ya U21, anatajwa kama mrithi wa kudumu wa Antonio Valencia.
 
7. KYLE WALKER
Mwanzoni, sikuelewa ni kwanini mwaka 2017 Pep Guardiola alikubali kuwapatia Tottenham Hotspur Euro 56 milioni kwa ajili ya huduma za beki huyu wa kati.
Lakini baada ya kumshudia akifanya alichokifanya pale Wembley Agosti 4 katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Liverpool, bila kushinikizwa niliamka kitini na kumpa saluti. Kyle Walker, nakuheshimu bro.
Haikuwa rahisi kwa mchezaji, wa kawaida kuokoa mpira ule wa Mohammed Salah katika mstari ule wa goli usiende wavuni. Ulihitajika mguu wa mtu kama Walker kumnyima Salah bao jioni ile.
 
5. AYMERIC LAPORTE
Beki mwengine wa kikosi cha sasa cha Manchester City, ni Aymeric Laporte, ambaye ni mmoja wa mabeki wanaopigiwa upatu kutikisa miaka ya baadae.
Laporte aliyebukia kwenye La Liga alikuwa anawindwa sana na FC Barcelona na walikuwa na uhakika wa kumpeleka Camp Nou, lakini Guardiola aliingilia kati.
Bila kigugumizi, bishoo huyo akatoa Euro 65 milioni, akampeleka Laporte Etihad. Juhudi hizi hazikuenda bure. Tangu asajiliwe Laporte amekuwa nguzo muhimu kwa City. usisahau na mabao yake.
 
4. LUCAS HERNANDEZ
Moja ya mabeki bora waliopikwa pale Atletico Madrid, chini ya mikono salama ya Diego Simeone, Lucas Hernandez, alitua Allianz Arena mara tu baada ya kutwaa Kombe la Dunia na taifa lake la Ufaransa mwaka jana.
Mapema mwaka huu, Lucas alipokea ofa nzuri kutoka Bayern Munich. Ilikuwa ni ngumu kukataa dili la Euro 80 milioni, hata Colchoneros wenyewe, waliona aibu kumzuia kuondoka.
 
Huyo tumeshamwondoa kabisa chamani [emoji23]
Jamani. Kwa nini bro?

Kama mnataka chama kirudi kwenye misingi sahihi nipeni uenyekiti chama kiwe transparent tuongeze wanachama. Haya mambo yenu ya simba mwendapole na kubebana na mizigo ya maua kila mwendako yanakiua chama [emoji16][emoji16][emoji16]
 
3. MATTHIJS DE LIGT
Kulikuwa na vita kubwa kati ya klabu kadhaa kubwa za Ulaya, zikiwania saini ya beki wa zamani wa Ajax, Mholanzi Matthijs de Ligt. Barcelona, Manchester United na Juventus zikiongoza.
Hata hivyo, mwisho wa siku, ni Juventus ndio iliyovunja benki na kufanikiwa kumpeleka Turin, ambako ameungana na Cristiano Ronaldo, kwa Euro 85.5 milioni.
 
2. VIRGIL VAN DIJK
Dunia ya soka kwa sasa inaongozwa na mabeki wa Kiholanzi. Kabla ya Agosti 02, Beki ghali zaidi kuwahi kutokea katika historia ya soka alikuwa ni beki wa Liverpool, Virgil van Dijk.
Van Dijk alitua Anfield mwanzoni mwa msimu uliopita kwa dili lililovunja rekodi ya dunia la Euro 86 milioni akitokea Southampton. Akamaliza msimu akiwa mchezaji bora wa EPL. Dunia nzima ilisimama na kumpa saluti.
Nahodha huyu wa Uholanzi, hakuiangusha mizimu ya Liverpool, iliyoridhia kusajiliwa kwake.
Hivi sasa anatajwa kama beki bora kabisa duniani na yupo katika tano bora ya wanaopigiwa upatu kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.
 
1. HARRY MAGUIRE
Hadi kufikia usiku wa Agosti mosi, beki ghali zaidi duniani alikuwa ni Mholanzi wa Liverpool, Virgil van Dijk. Ilikuwa ni ngumu sana kuwaza kuwa rekodi yake ya Euro 86 milioni, ingevunjwa haraka.
Lakini kumbe, Waingereza walikuwa na mpango. Haraka sana ikaanza kama uvumi.
Ghafla ikawa kweli, wakafanya figisu na kuhakikisha Harry Maguire anavunja rekodi ya Van Dijk.
Fumba na kufumbua, Mashetani Wekundu, wakatoa Euro 90 milioni kwa ajili ya saini ya Maguire. Wakati mchezo wa soka una maajabu yake Wallahi. Yaani leo, milioni 90 zinatoka kwa ajili ya beki? Hii ni kufuru au dharau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…