Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Haha

 
Kawaida bro,
Nilitegemea ningesherehekea nikiwa Burigi ila siunajua tena mambo yalivyoenda ....
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 bro unanifurahisha......

Burigi ilikua chungu sana ata mimi sikushauri kabisa 😂😂😂😂😂
Naona mnatengeneza menu bomba na pepsi hapo
IMG_20190816_065945.jpg
 
Mgonjwa mmoja nchini Uingereza amejikuta katika maumivu makali baada ya meno yake ya bandia kunasa kooni kwa wiki moja.
Mgonjwa huyo mwenye miaka 72 alikuwa akilalamika kupata maumivu makali wakati wa kumeza vitu na kukohoa damu katika kipindi chote hicho.
Bwana huyo, alimeza meno hayo wakati akifanyiwa upasuaji wa tumbo.
 
Undani wa tukio hilo umechapishwa kwenye jarida la kisayansi la BMJ ambapo watunzi wake wamewataka madaktari kuhakikisha wagonjwa wao wanaondoa meno ya bandia kabla ya upasuaji.
Siku sita tu baada ya upasuaji huo uliofanyika mwaka 2018, bwana huyo alienda kwa daktari na kulalamika kuwa nanashindwa kumeza vyakula vizito.
 
Madaktari awali waliamini kuwa hiyo ni athari ya kuwekewa mpira kwenye kinywa wakati wa upasuaji, na kumpatia dawa za kukabiliana na maumivu na maambukizi ya koo.
Lakini baada ya bwana huyo kurudi tena baada ya siku mbili akiwa na malalamiko zaidi, madaktari ikabidi wamfanyie uchunguzi zaidi wa koo.
 
Vipimo vya miale ya X-Ray vikaonesha kuwa kuna meno ya bandia matatu na chuma chake cha kuyashikilia.
Baada ya hapo, mzee huyo akawaambia madaktari kuwa alipoteza meno yake ya bandia katika kipindi ambacho alilazwa hospitalini kwa upasuaji wa tumbo.
Ikalazimika afanyiwe upasuaji wa haraka wa koo, lakini akarudi hospitali mara nne zaidi ili kuongezewa damu.
 
Watafiti wameeleza katika ripoti yao kuwa kuna zaidi ya mkasa mmoja wa watu kumeza meno ya bandia wakati wakipigwa dawa za usingizi.
Uwepo wa meno bandia ama kifaa chochote cha bandia kinywani, unatakiwa uripotiwe kabla nda baada ya upasuaji, wamesisitiza kwenye ripoti ya jarida hilo.
 
Hazel Stuart, ambaye ni mkurugenzi wa matibabu katika hospitali ya Chuo Kikuu cha James Paget ambapo upasuaji huo ulifanyika amesema uchunguzi wa kina ulifanyika juu ya tukio hilo.
"Baada ya tukio hilo, michakato yetu imepitiwa upya, na maboresho yamefanyika katika kila eneo la mahitaji, na tuliyojifunza tumehakikisha yanawafikia wafanyaki wetu wote ili kuepuka makosa," amesema.
 
Polisi katika mji wa Jos nchini Nigeria wanachunguza ni jinsi gani mvulana mwenye umri wa miaka 15 alivyodanganya kuwa ametekwa nyara na kuomba kikombozi kutoka kwa baba yake ili aachiliwe.
" Ni tukio lililofanyika kwa utalaamu ,"ameiambia BBC msemaji wa polisi - Terna Tyopev
 
Kijana huyo na marafiki zake wengine wanne wanaomzidi umri, ambao kwa sasa wamekamatwa na kuwekwa mahabusu ,walidai kikombozi cha naira 500,000 sawa na dola 1,365 , amesema
Walikuwa wamepanga kutumia pesa hizo kwa ajili ya sherehe za mahali ya kumaliza shule.
 
Siku tatu kabla ya kupanga utekeji nyara huo feki , bada yake na mvulana huyo alikuwa ameuza gari lake kwa ajili ya matumizi ya kifamilia.
Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 15 alipanga mpango huo baada ya kuisaka familia yake na kubaini kuwa pesa alizopata baba yake baada ya kuuza gari zilikuwepo.
"Pesa zilikuwa zimelipwa kwenye akaunti ya benki ya baba yake , kwa hiyo hazikuwepo ," Amesema Bwana Tyopev.
 
Marafiki zake walijifanya kuwa watekaji nyara wake na kuwasiliana na baba yake.
"Walimuonya kuwa mtoto wake amepelekwa mbali na Jos na kwamba hapaswi kuripoti kwa maafisa wowote wa usalama . Baba yake alifuata muongozo wao na aliripoti tu pale alipoona mambo yamekuwa hatari sana ," amesema msemaji wa polisi.
 
Back
Top Bottom