Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yajayo yanafurahisha(haka ka msemo voda wajinga sana wamekatumia kutupandishia gharama za vifurushi)
jamaa ameshajenga timu yake ya maangamizi japokuwa kuna watu walikuwa wanamdhihaki mwanzoni ila mjinga mimi nilikwishakifahamu anachokitafuta.

mtatiro
kitila mkumbo
mgombea uraisi wa ACT
mtolea brother
n.k

hii ni timu kubwa kuliko ya wapinzani wake wa ndani na nje.
20 years loading...........
 
DR AYOUB RIOBA

VOLCANO IKILIPUKA, WEMA NA WEHU WOTE SAWA.

Katika historia ipo miji mingi tu iliyofunikwa na volkano na kufutika katika uso wa nchi kwa sababu tu wakazi waliojenga pale hawakuwa na maarifa wala utaalamu wa kubaini chanzo cha volkano na hata kubaini kiwango cha madhara yanayoweza kusababishwa na mlipuko mkubwa na kutafuta ufumbuzi sahihi.
 
Mfano mzuri ni mji wa Pompeii na mji dada Herculaneum, huko Italia, ambayo mwaka 79 KK ilikumbwa na dhahama ya kufunikwa na kifusi cha volkano na kupotea kabisa katika uso wa dunia.

Kabla ya kukumbwa na dhahama hiyo, zilikuwapo nyakati wakazi wa Pompeii waliona moshi ukifuka katika Mlima Vesuvius, wao wakajadili moshi. Nyakati nyingine wakaona lava ikitiririka kutoka kileleni, wao wakajadili lava. Wakati mwengine wakaona moto ukilipuka kutoka kileleni wakajadili moto.
 
Wapo pia walioangaza macho yao kule kileleni na wakabisha kwa nguvu zao zote na kusema hakukuwa na moshi wowote na kwamba waliokuwa wakisema kuna moshi walikuwa wazushi tu ambao walitakiwa kupuuzwa. Wakasema waliosema kuna moshi walikuwa na nia ya kuvuruga amani na mshikamano wa wana Pompeii, na kwamba hawakuwa wazalendo.
 
Moto ulipoanza kulipuka wapo waliowajulisha wenzao kwamba mlima ulikuwa ukitema moto. Wapo waliosema ni miali ya radi tu. Wapo waliosema ule moto ulikuwa vimondo vinavyokatiza usiku. Na wapo waliotizama kileleni na bado wakasema hakukuwa na kitu chochote. Wakasema wanaoona moto milimani walikuwa wehu au wachochezi wanaoonea wivu kazi nzuri zinazofanywa na watawala wa Pompeii.
 
Siku volkano ilipoanza kulipuka hakukuwa na aliyebaki salama. Si waliokuwa sahihi wala walioita wenzao wehu. Wote waliangamia. Jamii ya Pompeii iliteketea kwa sababu haikuheshimu misingi ya maarifa kwa wenye kujua, badala yake iliendekeza hisia, tumbo na kujipendekeza kutatua matatizo yao, hivyo ilikumbwa na adhabu ya asili.!
 
Back
Top Bottom