Hivyo leo mimi na wewe hatuna haja ya kukimbia changamoto bali kuzikabili kwani ndani kuna njia ya kutokea au kufanikiwa ama muujiza kama Shigongo anavyouita.
Hivyo huenda ni muhimu pia kufahamu mambo ya kuzingatia kabla hujaanza safari ya kwenda huko ili usijutie pesa na muda wako. Anza kwa kuzingatia haya matano.
Kila mtu huingia huko akiwa na sababu tofauti na mwenzake. Wapo wanaokwenda kupunguza msongo wa mawazo, wanaokwenda kujipumzisha baada ya mizunguko ya siku, wanaokwenda kupata fursa mpya za kibiashara, wanaokwenda kusubiri foleni ipungue na ambao wao ni ratiba yao ya kawaida ya kila siku.
Kwa hiyo kabla hujaanza safari jiulize kwa nini nakwenda baa, kisha fanya tathmini ya baa unayotaka kwenda kama inaweza kuwa sehemu nzuri ya kufuata unachokitafuta vinginevyo utajuta.
Siyo kwa sababu wewe ni mlevi basi unatosha vigezo kuingia kwenye kila baa, utafeli. Ifahamu baa unayoingia ni ya daraja gani? La juu, la chini au la kati, kisha jitathmini na wewe ni mlevi wa daraja gani.
Kuna baa zinauza bia moja Sh15,000, ukiingia hizo wakati wewe ni wa bia za Sh2,500 unaweza kuagiza, ukanywa kama komba, halafu ukaletewa bili ya ajabu usiamini. Usipokuwa makini unaweza kupewa kazi ya kupanga makreti stoo.
Kiuhalisia hakuna mlevi aliyewahi kulewa hata akapasahau nyumbani kwake. Iwe isiwe, walevi wote hufika nyumbani hata baa iwe mbali kiasi gani. Yaani hata mtu anywe hadi azimie, atafika nyumbani hata kwa kubebwa. Kufika ni kufika.
Kila mtu anabadilishwa na pombe kuwa mtu fulani. Kuna wengine wakilewa wanakuwa wanamuziki, wataimbaa weeee mpaka mwisho. Wengine huwa waandishi wa habari, wengine huwa ‘usalama wa taifa’ na zaidi.
Wewe ukilewa unakuwa nani? Hili ni swali muhimu kujiuliza kabla hujaingia baa kwa sababu kwa mfano yawezekana ukilewa unakuwa Mike Tyson, unajisikia kupigana tu na kila mtu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.