Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Huzuni na anguko kuu la kinafsiya
Ni kubakia katika pango la Plato
Ukidanganywa na taswira butu za uhalisia
Ambao haujawahi kuwepo
Ni kweli nilikupenda?
Ni kweli ulijipenda?
Unapendeka?

929c9643-29b5-4eed-9f5b-7676067e166f.gif


The Don laivu ndani ya Koromije [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Ewe binti mwema
Uliyeumbwa kwa namna ya ajabu
Malaika mchanga asiye na mawaa
Tabia zako njema zimevuma sana
Mpaka huku Koromije zimetufikia
Urafiki wako wa thamani
Ubinadamu wako wa kupigiwa mfano
Umekutangulia nkoyi

Niruhusu basi hivi karibuni
Nichochee zeze langu
Kisha nisimame katika kilima chetu
Walipozikwa mashujaa wa ukoo wetu
Nighani sifa zako nizijuazo
Ili nikutambulishe rasmi
Karibu [emoji7][emoji7][emoji7]


c75fab4e-f495-4d61-a1bf-d37f6b0dcafd.jpeg
 
Ukweli ni kwamba kupunguza muda wa kulala hata kama ni kwa kiasi kidogo sana, kuna athiri kwa kiwango kikubwa sana juu ya jinsi mtu atakavyojisikia, nguvu za mwili, uharaka wa kufanya kazi wa akili na uwezo wa kukabiliana na msongo wa mawazo.
 
Ukiweza kujua kiusahihi mahitaji yako ya muda wa kupumzika na jinsi ya kurudia hali yako ya kawaida baada ya kipindi cha kukosa usingizi wa kutosha, utajipangia ratiba nzuri ya kupumzika na hivyo kuboresha maisha unayoishi ukiwa macho.
 
Kwa Nini Usingizi Ni Kitu Muhimu?



Kiwango na ubora wa usingizi unaoupata huathiri afya ya akili na ya mwili wako, na afya ya maisha yako ukiwa macho, vikiwa ni pamoja na uzalishaji wako katika kazi, hisia zako, afya aya ubongo na moyo, kinga za mwili wako, ubunifu, uchangamfu na hata unene wa mwili wako. Hakuna shuguli nyingine inayoleta faida nyingi kwa kiasi kidogo cha nguvu kama hivi.
 
Usingizi ni zaidi ya mwili wako kukata mawasiliano. Unapokuwa umepumzika, ubongo wako hubaki kazini, ukisimamia ukarabati unaotakiwa ili mwili wako urudi kwenye hali nzuri, tayari kukabiliana na shughuli za siku inayofuata.
 
Hauna jinsi ya kuchagua kati ya afya na uzalishaji kazini. Ukiweza kutafuta matatizo yako ya kupata usingizi wa kutosh kuyatatua na ukapata usingizi wa kutosha kila siku, uwezo wako wa kutenda kazi, ufanisi, na afya yako ka jumla vitaongezeka. Utapata matokeo zaidi katika siku moja kuliko ungefanya kazi kwa muda mrefu zaidi ukiwa umezongwa na usingizi.
 
Ukweli: Pengine hutasikia kusinzia mchana, lakini kukosa saa moja ya usingizi kunaweza kuathiri uwezo wako wa kufikiri vizuri na kukufanya uwe mzito katika kuchukua maamuzi yanayofaa. Vile vile kuna athari katika mfumo wako wa mishipa ya moyo na afya ya moyo, nguvu za mwili na uwezo wa mwili wako wa kupambana na maradhi.
 
Mwili huyazoea haraka mabadiliko ya ratiba zako za usingizi



Ukweli: Mwili huchukua zaidi ya wiki moja kurudia hali yake ya kawaida baada ya kusafiri na kuvuka kanda za muda (time zones) tofauti au kuingia shifti ya usiku kwenye sehemu yako ya kazi.
 
Unaweza kufidia usingizi ulioukosa katikati ya wiki kwa kulala zaidi wikiendi

Ukweli: Ingawa mpango huu unaweza kupunguza kwa kiasi fulani deni lako la usingizi, hauwezi kumaliza kabisa tatizo lako la kukosa usingizi. Isitoshe, ulalaji huu wa wikiendi unaweza kuvuruga mpangilio wa kusinzia-kuwa macho hivyo kwamba ikawa vigumu zaidi kupata usingizi kwa wakati mwafaka usiku wa jumapili na kuamka mapema siku za jumatatu.
 
Back
Top Bottom