Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unahitaji Usingizi Wa Saa Ngapi?



Kuna tofauti kati kubwa kati ya kiwango cha usingizi unachopata na kuwza kufanya kazi zako na kiwango halisi ulichostahili kukipata ili kufanya kazi zako kiufanisi. Watu wengi sasa hivi hupata chini ya saa 7 za usnigizi na kwenye dunia ya leo yenye changamoto nyingi za kimaisha saa 6 au 7 huonekana kama ni kiwango sahihi cha usingizi. Ukweli ni kuwa hii ni kujiweka kwenye hsli ya kuishia kwenye tatizo sugu la kukosa usingizi wa kutosha
 
Njia bora ya kujua kama unapata usingizi kwa kiwango cha kutosha ni kujitathmini jinsi unavyojisikia pale unapoanza shughuli zako asubuhi. Kama unapata usingizi wa kutosha, utajisikia kuwa na nguvu na mchangamfu siku nzima kuanzia ulipoamka hadi utakapokwenda kulala.
 
Biolojia Ya Usingizi



Ukiwa umelala, mwili wako unapitia kwenye mfululizo wa hatua mbalimbali zinazojitofautisha. Kila hatua kwenye usingizi ina lengo muhimu la kuboresha afya ya ubongo na mwili wako. Usingizini mwili unapitia hatua za kupishana za usingizi tulivu – quiet sleep, na kuota ndoto – REM (dreaming) sleep.
 
Hatua ya usingizi tulivu ni muhimu katika kuukarabati mwili, na usingizi wa ndoto ni muhimu kwa ajili ya kujifunza na kumbukumbu. Hatua hizi mbili ni tofauti kabisa kama kila moja ya hizo ilivyo tofauti na hali ya kuwa macho.
 
Wanasayansi wanaiita hatua ya usingizi tulivu kuwa ni “an idling brain in a movable body.” Katika hatua hii, kufikiri na shughuli nyingi za viungo hutulia, lakini miondoko ya mwili bado huweza kutokea, na mtu huweza kujisogeza wakati akiingia kwenye dimbwi zito zaidi la usingizi.
 
Tendo la kuingia usingizini ni la haraka sana ambalo ungeweza kulilinganisha na kuzima swichi ya umeme, maana yake au upo macho au upo usingizini. Kama hakuna kitu cha kukusumbua, utaingia taratibu kwenye hatua tatu za usingizi tulivu.
Hatua Tatu Za Usingizi Tulivu
 
Hatua ya Kwanza – Stage N1
Unapoingia kutoka kuwa macho hadi usingizi tulivu, unatumia kiasi cha dakika tano kwenye hatua ya kwanza -stage N1. Katika hatua hii, joto la mwili huanza kuteremka, misuli hulegea na macho hucheza taratibu kutoka upande mmoja hadi mwingine. Katika hatua hii, utapoteza ufahamu wa mazingira, lakini unaweza kuamshwa kirahisi.
 
Hatua ya Pili – Stage N2
Hatua hii ya usingizi halisi huchukua dakika 10 hadi 25. macho hutulia, mapigo ya moyo na upumuaji huwa chini ya viwango. Ubongo unafanya kazi bila mpangilio. Nusu ya muda unaoutumia kuwa usingizini, unakuwa kwenye hatua hii.
 
Hatua ya Tatu – Stage N3
Katika hatua hii mwili wako unaingia kwenye usingizi mzito. Upumuaji unakuwa na mpangilio zaidi. Msukumo wa damu huteremka na mapigo ya moyo kuteremka kwa asilimia 20 hadi 30. Ubongo hupunguza usikivu wa vitu vya nje na kufanya kazi ya kumwamsha aliyesinzia kuwa ngumu zaidi.
 
Back
Top Bottom