Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtiririko wa damu kuelekea kwenye ubongo hupungua, na ubongo hupoa kwa kiwango kikubwa. Mwanzoni kabisa mwa hatua hii, tezi ya pitutary hutoa homoni za ujenzi wa mwili ambayo itaamsha ujenzi wa tishu na ukarabati wa misuli.
 
Vijana hutumia asilimia 20 ya muda wao kuwa usingizini kwenye vipande vya usingizi mzito ambavyo huweza kwenda hadi nusu saa. Ni mara chache sana watu wa umri wa zaidi ya miaka 65 kupata usingizi mzito
 
Meja Jenerali Johnson Thomas Umunnakwe Aguyi-Ilonsi. Huyu alikuwa Mkuu wa Majeshi kwenye Serikali ya Balewa
Jenerali Ilonsi ndiye Mwanajeshi wa kwanza kufungua milango ya utawala wa mabavu nchini humo, baada mapinduzi ya umwagaji damu yaliyomaliza uhai wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Alhaji Abubakar Tafawa Balewa.
Aguyi-Ilonsi ni mtawala pekee wa kijeshi aliyedumu madarakani kwa muda mfupi kuliko wenzake waliofutia
Januari 15 1966 - July 1966
 
Ndoto huotwa kwenye kipindi cha usingizi wa ndoto (REM-rapid eye movement sleep), hatua ambayo huelezwa kama ni ya ubongo unaofanya kazi ndani ya mwili uliokufa ganzi (active brain in a paralyzed body).
 
Nafasi Ya Usingizi Wa Ndoto

Kama vile usingizi mzito unavyorudisha hali ya mwili, wanasayansi wanaamini kuwa usingizi wa ndoto huirudisha akili kwenye hali yake, labda kwa kufuta taarifa zisizo za maana.
 
Utafiti umeoonyesha kuwa mwanafunzi aliyepewa kazi ya kutoa majibu kwa swali linalohusu umbo gumu lisiloeleweka, akapewa nafasi ya kulala usiku mmoja, anakuwa na nafasi ya kutoa majibu mazuri zaidi kuliko yule aliyepewa swali hilo hilo kwa kushtukiziwa na kutakiwa kutoa majibu.
 
Utafiti wa zamani unaonyesha kuwa usingizi wa ndoto husaidia kujifunza na kumbukumbu. Watu waliotahiniwa kuona jinsi walivyolielewa jambo geni, walionyesha kufanya vizuri zaidi baada ya kupewa usiku mmoja wa kupumzika.
 
Wangeamshwa kila mara wanapoingia kwenye usingizi wa ndoto, mwongezeko huu wa ufaulu ungepotea. Kwa upande mwingine, wangeamshwa kila walipoingia kwenye usingizi tulivu, hakungetokea mabadiliko katika mwongezeko wa ufaulu wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…