Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tabia ya kusema hapana.
Hii ni moja ya tabia nzuri sana kwako wewe kuindeleza ili kufikia mafamikio. Unatakiwa kujifunza kusema hapana kwa mambo mengi sana. Unatakiwa ujue kusema hapana kwa wanaokupotezea muda wako au kwa yale mambo usiyoyahitaji.
 
Ikiwa wewe utakuwa ni mtu wa kukubali kila kitu, kwamba kitu hiki kiwe hivi au vile ni ngumu sana kuweza kupiga hatua sahihi za kimafanikioo husika. Jifunze kusema hapana kwa kila kitu ambacho hakina manufaa kwako wewe.
 
Tabia ya kuchukua majukumu yako.
Unatakiwa ujue kila mtu ana changamoto zake za kimaisha, lakini kama unashindwa kuwajibika na majukumu hayo na kila wakati kutaka kulaumu tu watu wengine, hilo tu nikwambie utakuwa ni miongoni mwa watu ambao watashindwa sana.
 
Nikwambie tu, kubali kuwajibika kwa kila jambo linalokuhusu wewe. Wajibika kwenye ndoto zako, wajibika kwenye maisha yako ya kila siku. Kila wakati ujue jinsi ya kuwajibika na hapo utaweza kupiga hatua za mafanikio sahihi kwako
 
Hivi ndivyo unavyoweza ukatumia tabia hizo vizuri na zikakusaidia wewe kuweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwenye maisha yako kama unavyotaka iwe. Ni jukumu lako wewe sasa kuchukua hatua na kuhakikisha unasonga mbele.
Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.
 
Kama Mambo Yako Yako Hovyo, Yaweke Sawa Kwa Kufanya Hivi.
Ikiwa kuna wakati unaona maisha yanakuchanganya hasa kutokana na changamoto unazokutana nazo, usije ukakubali ukafanya kosa la kuchanganywa huko, badala yake tuliza akili yako na tafuta mwelekeo sahihi wa maisha yako kwa kuweka mambo sawa.
 
Ikiwa unaona pia unaweka juhudi nyingi sana na juhudi hizo hazikupi matunda sahihi, hapa tena usikatishwe tamaa, endelea kuweka juhudi, lakini tafuta kuelewa kwa nini juhudi zako hazikufanikishi na anza kutafuta njia nyingine itakayokupa matokeo makubwa kwako na kuweka mambo sawa.
 
Upo wakati katika maisha yako ambapo kuna mtu au watu watakurudisha nyuma hata bila ya wewe kutegemea. Inapotokea wakati kama huu, sio swala la kutupa lawana na kusikitika, bali ni kuuvaa ujasiri na ushujaa na kutafuta mwelekeo upya kwa kuweka mambo yako sawa.
 
Kuna wakati katika maisha yako unajiona upo njia panda, huelewi hata ufanye nini, inapofika wakati huu , jifunze kuweka nguvu za uzingativu katika kitu kimoja na kutafuta mwelekeo sahihi utakaokusaidia kuweka mambo yako sawa na yakae katika mkao wa mafanikio.
 
Zipo nguvu nyingi na kubwa sana katika maisha yako, ambapo nguvu hizo zinauwezo wa kubali hali yoyote ambayo unayo na unaona ni mbaya na nguvu hizo hadi kukupa mafanikio halisi kama vile unavyotaka iwe.
Ndio maana, badala ya kulalamika na kutoa kila aina ya visingizio, jitahidi sana kuweka mambo yako sawa, kila unapoweka juhudi ya kuweka mambo yako sawa, utajifunza na kugundua kwamba kumbe unaweza ukatawala maisha yako kwa jinsi unavyotaka.
Je, katika maisha yako kuna kipi ambacho unakiona ndio tena basi kimeharibika na hakiwezi kukusaidia hata kufanikiwa. Kama kipo kitu cha namna hiyo, anza kikiweka sawa na kutafuta njia ya itakayofanya kitu hicho kikupe matunda uyatakayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…