Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

. Ndio maana hawa wenzetu kutetereka kitaasisi ni ngumu kwa sababu mfumo wao hauna muhali wala hauna mtukufu alie juu ya haki na sheria. Wanaweza kuwa na mkuu wa nchi mwenye ashki za upungufu wa akili lakini msingi uko imara na hauna muhali anapoteleza.
 
Yaani kama ingelikuwa kwetu yule mwanasheria alieipokea kesi hii kutoka kwa mteja wake na kumwakilisha mahakamani basi leo hii angelishafukuzwa uanasharia wake kwa kumkosoa kwa maneno makali Waziri Mkuu katika sakata hili la kuvunjwa bunge kinyume na sheria.
 
Mfumo wetu wa haki unatakiwa ujitathmini na haya yanayoendelea na jinsi gani wananchi wameanza kutokwa imani na chombo muhimu kwa maslahi ya nchi. Ndio usishangae ukawasikia wakuu wa wilaya na mikoa pamoja na mawaziri wakitishia kuua watu wakisema wazi kuwa mahakamani haki ni ngumu kupatikana. Na huu ndio mwanzo wa β€œjungle law” na ile tamthilia ya porini ya β€œSurvival of the fittest.”
 
Kwa ufupi Mahakama na bunge ni mihimili inayojitegemea na yenye nguvu huru baina yao na serikali. Msingi wa kuwa na mihimili hii huru ni kihakikisha haki inasimama (check and balance). Hakuna mzizi mkuu dhidi ya mahakama. Wala mahakama haiwezi kuona haya kuweka maamuzi ya haki pale ambapo spika wa bunge anafanya makosa yanayodogosha haki na kuenda kinyume na sheria.
 
Leo mahakama imeingilia kati kesi ya kufungwa bunge ambapo Waziri Mkuu anakemewa kwanza kwa kumshauri Malkia kufunga bunge kinyume na matakwa ya sheria na halkdhalika inalifungua bunge liendelee na kazi ya uwakilishi thabit wa wananchi katika demokrasia. Imeingilia kati kwa sababu kazi ya mahakama ni kuweka haki penye mashaka, haina aliejuu, haina wa kumuangukia au wa kubeba amri kutoka juu.
 
Jnr Farrell
September 11 at 9:51 PM Β·
#AfrikaVBrexit

Ndio huko nyuma nikasema kwa muafrika hasa wale commonwealth suala la Brexit walitazame kwa maslahi ya waafrika wageni wenzao badala ya kuwekwa katika kapu moja la uenyeji tusio nao.

#Elimu

Wanafunzi wa kiafrika wanaokuja kusoma UK kwa sasa hawafaidiki na chochote zaidi ya elimu pekee. Na kubwa zaidi gharama za elimu kwa mwanafunzi mmoja wa kiafrika ni maradufu ya mwenyeji, yaani mwananfunzi mwenyeji analipa paund za muingereza kati ya 4000 mpaka 6000 lakini mgeni analipa si chini ya paund 12000 za ada tu mbali sasa na za kujikimu, makaazi na gharama nyengine za kuishi ugenini.
 
#Fikiri

Hesabu ya rahisi ni kuwa muafrika mgeni anawekeza hapa kwa mwaka mmoja wa elimu yake si chini ya paund 35,000 huku akikabiliwa na changamoto za kuzuiwa kufanya kazi. Huko nyuma kabla ya ongezeko kubwa la nchi wanachama kujiunga na Umoja wa Ulaya hadhi ya mwanafunzi wa kigeni ilikuwa kubwa na serikali ikitambua umuhimu wao kwa uchumi wa nchi yao. Mwanafunzi aliruhusiwa kufanya kazi kwa kadri ya uwezo wake alimradi asifeli.
 
#Gharama

Katika uonevu mkubwa wa kibepari ni hili suala la mwanafunzi wa kigeni asiruhusiwe kufanya kazi na kutakiwa gharama zake zote za kuishi na kusoma nchini alipe mwenyewe kutokea kwa anaemdhamini. Hili likituathiri zaidi wa Afrika na limepunguza sana wanafunzi wa kiafrika katika sekta ya elimu hasa Uingereza. Zamani ukipata mdhamini wa ada na vijipesa kidogo vinatosha kujiendeleza kwa kufanya kazi na kujigharamia mwenyewe.
 
#Ukoloni

Kwa sasa ni tafauti, ni ukoloni maana unakuja na chako chote na huna unachoondoka nacho badala ya cheti ulicholipia. Unapozuiwa kufanya kazi maana yake kila hitajio lako lazima livuke bahari, na ndio msingi wa kuuita ukoloni maana mwanafunzi mmoja anatoa ajira za wenyeji kipato cha chini cha sawa na watu wawili mpaka watatu kwa mwaka. Unatoka na 35,000 kila mwaka kunufaisha uchumi wa mwengine badala ya alau nawe kunufaika na kidogo katika fursa kubwa ya kiuchumi walio nayo. Zuio la ajira linakandamiza ustawi wa uono na kuendelea kudumaza fikra za wanafunzi wageni. Ajira na elimu ziendane ili unufaike badala ya elimu pekee tena ya mamilioni kulipwa kutoka nchi masikini kuenda kwa tajiri, mantik gani kama si uonevu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…