Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

aliwahi kuandika Humble African
King Tutankhamun; Roho ya Farao (Mummy) iliyowamaliza watu kwa laana yake kali.

Kwa nchi ya Egypt kama kuna Farao alieitikisa Misri akiwa hai na na kuendeleza ubabe hata akiwa mfu kaburini basi alikuwa ni mtoto mdogo aliejitwalia ufalme akiwa na miaka tisa tu kutoka kwa baba yake aliefariki then ufalme kuhamishiwa kwa mtoto wake mdogo kabisa wa kiume aliezaliwa mwaka 1325 kabla ya yesu kuzaliwa na kuzikwa mwaka 1334 aliefahamika awali kama Tutankhaten huku neno Aten likiwa na maana "the living face of sun God"
 
Mungu ambae baba yake alikuwa akimuabudu ambapo baada ya baba yake kufariki alibadilisha jina na kuitwa tutankhamun huku neno Amun likiwa na maana "the living face of all God" na hii ni baada ya yeye kubadilisha namna ya kuabudu katika utawala wake huo ikiwemo hata kuabudu kulikopelekea na majina kubadilishwa nchini Misri kuanza kuishia na neno "Amun" ikiwa na maana "the living face of all God". Mfano "Tuta nkh Amun"
 
Na kwa vile aliunyaka uking akiwa na umri mdogo magenerals na washauri wake walimsaidia sana kuiongoza Misri ambayo ilikuwa himaya yenye uthabiti na ubora wa hali ya juu sana kivita, kiutawala, kidini n.k kipindi hicho ilikuwa Misri iliyoteka sehemu ya Nubia empire iliyokuwa na akiba ya dhahabu kibao walizoiba na kujiwekea Kama hazina nchini mwao Misri
 
isitoshe hata sehemu za Mediterranean walifanikiwa kuziteka na kuzitawala. Iliwatisha wananchi kuona mtoto wa miaka tisa anaongoza taifa kubwa kama Misri kwa wakati huo Misri ikiwa yenye ushawishi Duniani ila Jenerali mkakamavu Aye alimsaidia King Tut kuiweka himaya sawa na imara bila kutetereka.
 
Katika kile kipindi wafalme walioana Dada na kaka ili kulinda ule ufalme usitoke nje ya koo yao hivyo hata wazazi wa king Tut walikuwa kaka na Dada kitu kilichopelekea awe na matatizo makubwa ya kiuumbaji yakifahamika kama genetical disorder ambapo alikuwa na mguu moja uliopooza, meno yasiyo na formula, hips pana kama za kike, e.t.c
 
hakudumu muda mrefu kwenye utawala maana alitawala kwa miaka 9 pekee na baadae akafariki na sababu za kifo chake hazikufahamika wazi wazi ingawaje kuna nadharia zinasema alikufa kwa ajali ya kunagushwa na farasi wengine wanasema alikufa Kwa maralia... Ingawaje kuna kovu kichwani mwake ambalo wataalamu wa 3D Scanning wanadai alilipata baada ya kuwa ameshafariki.
 
Kifo chake ilikuwa mshtuko mkubwa kwa Misri maana hakuna alietegemea kama King atakufa katika umle mdogo kama ule na kwa vile hakukuwa na maandalizi yeyote muhimu juu ya kifo chake ikiwemo kuandaa kaburi lake mfalme kama inavyojulikana kipindi cha zamani watu wenye nafasi na pesa kwenye jamii walikuwa wanaandaa makaburi yao mapema
 
kabla hawajafa ili wakifa wakazikwe humo na makaburi yalikuwa ni miamba wanachimba chini yanakuwa na vyumba vikubwa zaidi hata ya 10 na kimoja ndio kinakuwa kaburi vingine wanaweka Mali na vitu vyake atakavyoambatana navyo huko anakoenda kwenye after life kwa mujibu wa imani zao waliamini atahitaji hivyo vitu huko kwenye maisha ya baadae...mfano Yesu alipofariki kuna tajiri alijitolea kuuzika mwili wa yesu kwenye kaburi lake mwenyewe alilotakiwa kuzikwa yeye kutokana na udharula wa kifo cha Yesu
 
Kwa ishu ya king Tut bahati mbaya hakuandaliwa kaburi lake maana alifariki ghafla hivyo akaamriwa jamaa mmoja aliekuwa official atoe kaburi lake ili kingTut akapumzishwe.. Maana moyo ulikuwa umeanza kuharibika na kwa mujibu wa imani za Wamisiri wa kale waliamini moyo ndio kiungo muhimu sana kwa binadamu kwenda nacho kwenye after-life maana ndicho anachotumia kufikiria na kureasoan mambo na kuchakata taarifa.. ubongo kwao ulikuwa kiungo cha kawaida sana hawakuamini kama binadamu anafikiria kwa kutumia kichwa.
 
usiku mmoja nimelala nilitafunwa na mdudu tandu tena karibu na sehemu ya makalioni nikiwa maeneo fulani, ebwana wee nilikuwa natembea ovyo kama baradhuli wa malindi anayetoka kupewa huduma na mabaharia wa kiarabu.
sikupata tena usingizi siku hiyo.​
[emoji23][emoji23][emoji23]
Huwa unanifurahisha na comment zako
 
fahamike kwamba huyu mfalme mtoto alikufa kipindi ambacho Misri ilikuwa kwenye ubora wake na ilikuwa na mali nyingi sana ilizoiba Duniani kama dhahabu, almasi n.k hivyo king Tut alivyokufa akazikwa kwenye hilo kaburi huku vyumba viwili chini ya huo Mwamba wa kaburi kukijazwa Mali zisizo kifani zikiwemo kiti chake cha ufalme cha dhahabu tupu, mask yenye sura yake ya kifalme ya dhahabu, jeneza lake alilolazwamo lilikuwa la dhahabu, fimbo zake za ulemavu zaidi ya 130 zilikuwa nyingi za dhahabu, sandals zilizokuwa na sura ya maadui zake kwenye soli kama ishara ya kuwakanyaga, nyoka wake wa dhahabu na masanduku makubwa ya dhahabu tupu na Mali zingine kibao za kufuru..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…