Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hahah sawa sawa binti mpole, umeeleweka vyema

#sautiiposawa
 
-kama watu wanataka kuondoka kwenye maisha yako waache waende.

usilazimishe watu wakupende wakujali au wawe pamoja nawe kwenye shida au wawasiliane nawe au wahisi maumivu na masumbuko yako ikiwa hawafanyi hivyo.

lazima ujue mwisho wa kitu ukifika haijalishi umekutana nao wapi na vipi na ni muda mrefu kiasi gani toka ukutane nao.
 
jifunze kuwaachilia.

MUNGU anayefanya njia kwenye bahari na mahali pa kupita kwenye maji ya nguvu Anajua ulipo na Anajua ulipokwama

Anamuita ndege mkali kutoka mashariki na mtu wa shauri lake kutoka nchi ya mbali tena Atoa watu kwa ajili yako na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.

Ameandaa watu wa kukusaidia watu ambao tayari wamewekwa TAYARI TAYARI wakikusubiri ili kukusukuma kuifikia hatima ya maisha yako ili kukusukuma kulitimiza kusudi la MUNGU angali uko hai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…