Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

I see, pole sana.
 
Mariyan Ognyanov: (Miaka 18 na siku 59)

Miezi miwili tu baada ya kutimiza miaka 18 staa huyu wa Levski Sofia alifunga bao lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya katika pambano dhidi ya Chelsea msimu wa 2006/07. Bao hilo lilikuwa la kufutia machozi wakati timu yake ikikumbana na kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa wababe hao wa England. Mpaka sasa hajafunga tena bao katika michuano hiyo na Levski mpaka leo haijawahi kufuzu tena michuano hiyo.
 
Alex Oxlade-Chamberlain: (Miaka 18 na siku 44)

Kwa bao hili katika pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya msimu wa 2011/12, Alex Oxlade-Chamberlain alikuwa mchezaji mdogo wa Kiingereza kufunga bao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya. Ilikuwa ni dakika ya nane tu ya pambano lake la kwanza la michuano hii akiwa na jezi ya Arsenal dhidi ya Olympiakos. Ndio kwanza alikuwa amejiunga na Arsenal akitokea Southampton huku akifurahia mechi hizo kwa sababu Arsenal ilivuka mpaka hatua ya 16 bora ambapo ilitolewa na AC Milan.
 
Karim Benzema: (Miaka 17 na siku 355)

Staa huyu wa sasa wa Real Madrid alifunga bao lake la kwanza la soka la kulipwa katika pambano la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Rosenborg ya Sweden akiwa na jezi ya Lyon msimu wa 2005/06. Hata hivyo, baadaye Lyon walitolewa katika hatua ya robo fainali na AC Milan huku Benzema akiwa ameacha jina kubwa katika soka ambalo baadaye lilimpeleka Real Madrid anakocheza hadi sasa.
 
Aaron Ramsey: (Miaka 17 na siku 299)

Katika pambano hili la Ligi ya Mabingwa wa Ulaya dhidi ya Fenerbahce msimu wa 2008/09 bao lake lilimfanya staa huyu wa Wales kuwa mchezaji wa pili aliyezaliwa miaka ya 1990 kufunga bao katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya. Arsenal waliichapa Fenerbahce ya Uturuki mabao 5-2 na na kutinga nusu fainali ambapo walitolewa kwa jumla ya mabao 4-1 na Manchester United.
 
Breel Embolo: (Mabao 17 siku 263)

Mshambuliaji huyu wa Uswisi alifanikiwa kutangaza jina lake duniani akiwa na umri wa miaka 16 tu wakati alipofunga bao katika dakika ya nne tu ya pambano la timu yake ya Basel dhidi ya Ludogorets msimu wa 2014/15. Msimu huo kwa ujumla alifunga mabao 17 huku Basel wakitolewa na Porto katika hatua ya 16 bora kwa jumla ya mabao 4-0.
 
Martin Klein: (Miaka 17 na siku 240)

Jina lake sio maarufu sana kwa mashabiki wa soka lakini anabakia kuwa mchezaji wa tano mdogo kufunga katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Ulaya. Ilikuwa ni katika pambano kati ya timu yake Sparta Prague ya Czech dhidi ya Panathinakos msimu wa 2001/02. Bao lake lilikuwa la kufutia machozi wakati Sparta wakichapwa mabao 2-1 lakini atalikumbuka kwa muda mrefu zaidi katika msimu ambao walishindwa kusonga mbele hatua ya makundi huku mabingwa wakiwa Real Madrid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…