Zlatan Ibrahimovic (48)
Zlatan Ibrahimovic amezurura kwenye timu nyingi sana huko Ulaya akipita Ajax, Juventus, Inter, Barcelona, AC Milan, Paris Saint-Germain na Manchester United, ambako kote alizotumikia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwenye michuano hiyo, bao lake la kwanza alifunga wakati Ajax ilipoitandika Lyon 2-1, Septemba 17, 2002. Katika mchezo huo, Ibra alifunga mabao yote mawili katika mechi yake ya kwanza kabla ya kuja kufunga 46 mengine katika kipindi cha miaka 14 aliyotamba katika timu kibao za huko Ulaya kabla ya kutimkia Marekani. Mechi zake za mwisho katika michuano hiyo zilikuwa kwenye msimu wa 2016/17.