Sheria ya makosa ya mtandao mbona iko wazi kuhusu kosa alilotenda? Wanaenda kupekua nyumbani kwake ili iweje? Wanatafuta kopmyuta aliyotumia kufanyia hiyo photoshop?
Halafu sheria ile inatungwa na kupitishwa tupo tunaona hivi. Wakati huo mi nilikuwa na blog moja pendwa sana tukijadili siasa, ishu za maisha na mambo ya kifalsafa na elimu. Wengi tuliamini kuwa sheria ile JK asingeitia sahihi bila marekebisho yaliyokuwa yamependekezwa kwa sababu alikuwa na rekodi nzuri sana kuhusu uvumilivu wake dhidi ya vyombo vya habari. Wengi tulishangaa alipoitia sahihi na nadhani mpaka leo wachambuzi wengi wanaamini kuwa hili lilikuwa ni kosa mojawapo kubwa ambalo si ajabu mpaka leo analijutia (kama wanasiasa huwa wanajuta)
Umekuja utawala huu sasa ikawa hata kuendesha blog ikawa mpaka ulipie. Dola 900+. Nilidelete blog yangu yenye watembeleaji zaidi ya 15 milioni (tena wabobevu wanaojielewa na siyo wafakamia urojo kama
Daemusin) kwa shingo upande na mpaka leo nina hasira na jambo hili ndo maana hata kushiriki mijadala mizito sina motisha kabisa.
Ni mwendo wa kula likes tu na sembe aisee. Hovyo kabisa !!!