Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hapana huyo mwenye chura ni tishio mtaani tu.
Mahakamani hii ni kesi nyepesi sana.
Atachomoka tu kama hatobambikwa kesi ingine tusiyo ijua.
Sheria ya makosa ya mtandao mbona iko wazi kuhusu kosa alilotenda? Wanaenda kupekua nyumbani kwake ili iweje? Wanatafuta kompyuta aliyotumia kufanyia hiyo photoshop?

Halafu sheria ile inatungwa na kupitishwa tupo tunaona hivi. Wakati huo mi nilikuwa na blog moja pendwa sana tukijadili siasa, ishu za maisha na mambo ya kifalsafa na elimu. Wengi tuliamini kuwa sheria ile JK asingeitia sahihi bila marekebisho yaliyokuwa yamependekezwa kwa sababu alikuwa na rekodi nzuri sana kuhusu uvumilivu wake dhidi ya vyombo vya habari. Wengi tulishangaa alipoitia sahihi na nadhani mpaka leo wachambuzi wengi wanaamini kuwa hili lilikuwa ni kosa mojawapo kubwa ambalo si ajabu mpaka leo analijutia (kama wanasiasa huwa wanajuta)

Umekuja utawala huu sasa ikawa hata kuendesha blog ikawa mpaka ulipie. Dola 900+. Nilidelete blog yangu yenye watembeleaji zaidi ya 15 milioni (tena wabobevu wanaojielewa na siyo wafakamia urojo kama Daemusin) kwa shingo upande na mpaka leo nina hasira na jambo hili ndo maana hata kushiriki mijadala mizito sina motisha kabisa.

Ni mwendo wa kula likes tu na sembe aisee. Hovyo kabisa !!!
 
Sheria ya makosa ya mtandao mbona iko wazi kuhusu kosa alilotenda? Wanaenda kupekua nyumbani kwake ili iweje? Wanatafuta kopmyuta aliyotumia kufanyia hiyo photoshop?

Sina hakika mahali anakofanya kazi zake Idris,
Kwa swala la Computer anayoitumia nadhani wangekwenda Ofisini kwake.

Swap ya Faces kwa Photoshop na aina ya kazi anazofanya Idris hazimfanyi kuwa na hatia.
Hii ndio sababu nadhani ya search ili kumtia nguvuni.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sio wafakamia urojo kama nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…