Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

17933785_1102354386575920_1141760173094731776_n.jpg
 
Kuna jamaa mmoja zamani tuliwahi kuishi naye mtaani, mitaa ya zamani ya Yegomasika.
Huyu bwana alikamatwa nchini Sweden baada kufanya kosa ambalo kwa hapa kwetu unakula miaka kuanzia 15 gerezani na kazi ngumu, huyo ndugu ambaye hivi sasa ni marehemu, alifungwa miaka 4 bila kazi za maana na siku alipotolewa jela amepewa bonus za kutosha pamoja na $ 4,000 keshi.[emoji23][emoji23][emoji23]
Nadhani falsafa yao ya magereza siyo kumwadhibisha mfungwa bali kumbadilisha tabia (rehabilitation). Bila shaka kuna programu nyingi kielimu na hata kitaaluma-tendaji ili kumpatia mfungwa huyo nyenzo za kumsaidia siku akitoka gerezani. Mifumo ya aina hii inahitaji uwekezaji sana na jamii iwe imeandaliwa vyema kubeba hizi gharama kubwa za kuwabadilisha hawa wafungwa.

Norway, kama zilivyo nchi nyingine za Skandinavia, ina huduma bora sana za kijamii na inashika nafasi za juu katika indexes za kila mwaka za mataifa yenye watu wenye furaha na ridhiko. Pia ina kiwango kidogo sana cha ufisadi na uhalifu wa kutisha. Tatizo pekee ni kodi kubwa sana ambazo hasa, ndiyo hugharamia huduma hizi bora za kijamii tunazoziona mpaka kwa hawa wafungwa. Na naamini kuwa hawa ni wafungwa wa makosa madogo madogo ya kawaida. Sidhani kama wafungwa wa makosa ya kutisha kama mauaji na ubakaji wanaishi maisha ya aina hii.
 
Back
Top Bottom