Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wa forex bado ana wafuasi wengi wanaomtetea. Ukitaka kumuibia mtanzania na akuone tapeli mjanja na asiumie kama umemtapeli mtafsirie vitabu vya kizungu kwa style ya gazetireeefuuuu,mpe mamifano ya kila aina ya matajiri wakubwa.
 
Sote tunafahamu kwamba tumbaku ,unene wa mwili kupita kiasi na ukosefu wa mazoezi vinaweza kuongeza uwezekano wako wa kupata kiharusi.

lakini kuna mambo mengine ambayo huenda hujawahi kuyasikia yanayoweza kusababisha maradhi hayo.

Maradhi ya moyo yanaongoza kwa kusababisha vifo kwa mujibu wa data zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
 
Moyo hushukuru unaposafisha meno yako
Meno yetu na mioyo yetu vina uhusiano mkubwa.

Uchunguzi kadhaa umeonyesha kuwa wenye afya mbaya ya kinywa wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo ya moyo.

Fizi zenye majeraha huwawezesha bakteria kuingia kwenye mfumo mzima wa damu.

Zinaweza kusaidia kukwama kwa mafuta kwenye mishipa ya damu.
 
Zinaweza pia kusababisha ini kutengeneza viwango vikubwa vya aina fulani za protini ambazo hujeruhi mishipa ya damu.

Vidonda hivyo hatimae vinaweza kusababisha mshituko wa moyo au kiharusi.

Je kuna suluhu? piga mswaki na tumia uzi kusafisa mianya iliyopo kati kati ya menona mtembelee daktari wa meno
 
😁😁😁😁😁😁Mjini shule, shamba kilimo.
 
Si jambo la mzaha - kumchukia bosi wako kunaweza kukusababishia matatizo ya afya ya moyo.

Utafiti uliofanywa kwa miaka 10 nchini Uswisi na kuchapishwa kwneye jarida la tiba la Uingereza- British Medical Journal ulibaini kwamba uhusiano mbaya na kiongozi wako kazini huongeza uwezekano wa shinikizo la damu kwa asilimia 40% ya watu.
 
Kiharusi kinaweza kusababishwa na msongo wa mawazo kazini," anasema Vijay Kumar, daktari bingwa wa moyo katika taasisi ya afya ya moyo ya Orlando nchini Marekani.

Pamoja na sababu nyingine kama vile kutopata usinginzi wa kutosha na chakula kisichofaa husababisha uwezekano wa maradhi hayo hata zaidi.
 
Tukio la kushitua linaweza kukusababishia kiharusi
Taarifa ya ghafla inayokushitua mfano kifo cha mtu wa familia yako inaweza kukusababishia kiharusi.

Kwa mujibu wa shirika la afya ya wanawake waliotimiza umri wa kutoweza kupata ujauzito nchini Marekani , mishipa ya damu miongoni mwa wanawake ambao wamewahikupitia matukio matatu ya kushitua maishani mwao, uwezo wao wa kufanya kazi ni mbaya wakilinganishwa na wanawake ambao hawajawahi kupitia uzoefu huo.
 
Upweke unaweza kuathiri vibaya moyo wako
Jarida jingine la kitabibu la Uingereza linaonyesha kuwa watu wenye mahusiano ya kijamii na watu wachache wanakabiliwa na uwezekano wa asilimia zaidi ya 29% ya kupatwa na maradhi ya moyona asilimia 32% zaidi ya uwezekano wa kupata kiharusi.
 
Moja ya sababu za athari za za upweke ni kwamba husababisha msongo wa mawazo na watu walio na upweke hawana mtu wa kuwasaidia kukabiliana na hisia zao.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Oxford na kuchapishwa mwaka 2014 uliowahusisha wanawake zaidi ya 700,000 kwa zaidi ya miaka minane, ulibaini kwamba watu wanaoishi na wenzi wao walikuwa na uwezekano wa chini ya asilimia 28% wa kufa kwa maradhi ya moyo kuliko wanawake wanaoishi peke yake.
 
Msongo wa mawazo unaweza pia kuathiri afya yako ya mwili.
Shirika linalojishughulisha na masuala ya afya ya moyo linasema kuwa 33% ya wagonjwa wa shinikizo la damu nchini Marekani hupata ugonjwa huo kutokana na msongo wa mawazo.

Wataalamu wanashuku kwamba watu wenye matatizo ya afya ya akiliwanaweza kuhisi ugumu wa kuchukua maamuzi ya kiafya.

Nieca Goldberg, mkurugenzi katika kituo cha afya ya wanawake cha New York cha Joan H. Tisch, anasema tabia kama ya kula chakula chenye virutubisho vya mwili au kuwa na kikomo cha kiwango cha unywaji wa pombe inaweza kuwa ni jambo gumu kwa watu wenye msongo wa mawazo.
 
kupungua kwa homoni kunakosababishwa na kipindi cha kutoweza kupata ujauzito huathiri mfumo wa moyo wa mwanamke
Wanawake wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kupata shinikizo la damu katika miaka ya baada ya kipindi cha kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito.

huenda hii ikawa na uhusiano na kupungua kwa homoni asilia za uzazi katika miili yao.

inaaminiwa kuwa homoni aina ya estrogen zina athari chanya kwenye kuta za mishipa ya damuj inayosaidia afya ya mishipa ya damu.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Jackie Eubany anaongeza kuwa umri huifanya mishipa ya damu kukakamaa jambo linalosababisha msukumo wa kiwango kikubwa wa damu.

Hata hivyo, lishe bora na mazoezi ya mwili ya mara kwa mara vinaweza kusaidia kukabiliana na athari hizo.
 
Usinipunguzie umri wangu mkorea, mi ni mmoja kati ya wahenga wachaache hapa.
Wakati Gerd Muller anakabidhiwa Kombe la Dunia baada ya mechi ya kibabe dhidi ya Uholanzi mwaka 1974, mi tayari nipo Duniani ingawa nilikuwa mdogo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
nimeanza kukuogopa mtani wangu.
huenda umri wako ni kuanzia miaka 33 kwenda juu.

kama ni kweli basi napaswa kupunguza utani wa kijinga dhidi yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…