Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1573882157123.jpeg
 
Mapenzi ya dhati

Huwezi ukakosa swala la mapenzi ya dhati kwa timu pamoja na mchezo wenyewe kwa shabiki yeyote yule wa mpira wa miguu.

Mashabiki wa mpira wa miguu wameonyesha mapenzi makubwa kwa ajili ya timu zao kiasi cha kuzitaja na kuzielezea hadharani, kuzichangia, kumiliki vitu vinavyotangaza timu husika, kutoa muda wao, n.k.

Kwa hakika unaweza kujifunza kupenda na kufanya kwa moyo kitu chochote unachokifanya ili kifanikiwe.
 
Kukosa aibu

Shabiki halisi wa mpira wa miguu kuvua nguo uwanjani au kupiga kelele za kushangilia siyo jambo la aibu. Kila shabiki halisi hufanya kila analoweza bila kujali aibu ili tu ahamasishe timu yake kushinda kwa njia ya kuishangilia.

Kwa hakika katika maisha ya kawaida pia ni muhimu kutokuona aibu katika kutekeleza mambo mbalimbali ili tufanikiwe.

Kumbuka kuwa wapo watu walioanza kufanya kazi za aibu lakini sasa wana kazi na maisha mazuri kwa sababu hawakuona aibu kufanya kazi zinazoonekana kuwa ni za aibu.
 
Kuwa mtafiti

Kila mara utawakuta mashabiki wa mpira wa miguu wakiwa karibu na redio, televisheni au intaneti ili kuchunguza na kupata taarifa mbalimbali zinazohusu timu mbalimbali, wachezaji, uchambuzi, utabiri wa matokeo, n.k.

Kuna mtu anaweza kukuelezea mambo ya timu za Ulaya hadi ukafikiri naye yuko huko au ametoka huko hivi karibuni; lakini hii ni kutokana na kutafiti bila kuchoka juu ya maswala ya mpira wa miguu.

Pasipo shaka unaweza kujifunza juu ya kuwa mtafiti kutoka kwa mashabiki wa mpira wa miguu ili uongeze maarifa yako.

Kumbuka kadri unavyokuwa na maarifa ya kutosha katika kile unachokifanya ndivyo unavyoongeza nafasi ya kufanikiwa zaidi.
 
Imani ya kushinda

“Kwa kawaida tunakuwa kile tunachoamini au kufikiri.”
Haijalishi timu imeshindwa mara ngapi au imekosa viungo muhimu wangapi, bado mashabiki wataamini kuwa timu yao itashinda.

Ni muhimu kuwa na imani ya kufanikiwa au kushinda katika jambo lolote tunalolifanya ili lifanikiwe hatakama kuna changamoto nyingi.
 
Juhudi na kujitoa

Mashabiki wa mpira wa miguu hukesha, hulipa pesa au hata kusafiri umbali mrefu ili kushuhudia timu yao ikicheza. Hawajali gharama wala maumivu, wao hujitoa kwa moyo na kwa juhudi nyingi ili kuishuhudia na kuiwezesha timu yao kushinda.

Hakuna jambo lolote linaloweza kufanikiwa bila juhudi na kujitoa. Ni muhimu kujifunza jambo hili na kuliweka katika matendo kwenye yale unayoyafanya. Fanya kazi kwa bidii usiku na mchana hadi uone malengo yako yakitimia.
 
Kujali muda

Hakuna shabiki wa mpira wa miguu anayetaka kuchelewa kwenye mpira. Nakumbuka wakati nikiwa chuoni watu walikuwa wakiwahi viti kwenye ukumbi wa mpira saa mbili kabla ya mpira kuanza.

Mashabiki wa mpira wa miguu hufanya kazi zao mapema na kwa juhudi ili wasije wakachelewa au kazi hizo zikawazuia kutazama mchezo wa timu zao.

Kwa kuwa kila jambo limefungwa kwenye muda; ni muhimu kuhakikisha unazingatia matumizi mazuri ya muda ili ukamilishe malengo yako. Usipoteze muda kwenye mambo yasiyokuwa na msingi wowote.
 
FAIDA ZA KUANGALIA TAMTHILIA(MOVIE)
ZIFUATAZO NI FAIDA ZA KUTAZAMA/KUANGALIA MOVIE/TAMTHILIA

SOMA NA UJIFUNZE

1.KUONGEZA HARI

2.KUSHAWISHI (mambo mema

3.KUTULIZA AKILI

4.KUKUKUMBUSHA NYAKATI (kama uliangalia wakati wafurahaa basi kila utakapoangaliautakumbuka)

5.KUKUPA HISIA FULANI

6.KUBURUDISHA

7.KUHIMIZA (psychological power)

8.KUFUNDISHA

9.kukupa nguvu pale unapokata tamaa
 
JE WAJUA,,,,
1.Kila siku na kila mtu anaona nyota mpya moja! yaani wewe apo kila siku kuna nyota mpya moja unaiona sasa piga hesabu ni siku ngap umeshaishi pia fanya hesabu watu wote duniani wanaona nyota mpya kila siku na watu wote waliowahi kuishi sayari ya dunia.🔺🔻
 
Back
Top Bottom