Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KAZI na pesa. Jose Mourinho ameambiwa akiipeleka Tottenham Top Four, basi atalamba Pauni 2 milioni bila wasiwasi. Hiyo ni bonasi yake binafsi. Siyo ya wachezaji wala benchi lake la ufundi. Hilo ndilo jukumu lake la kwanza kikosini.
 
Mourinho amesaini mkataba wa miaka mitatu na nusu na Spurs, na anatazamiwa kulipwa kiasi cha Pauni 15 milioni kwa mwaka, hivyo kuwa kocha wa pili anayelipwa zaidi katika Ligi Kuu ya England huku akilipwa mara mbili ya kile ambacho Pochettino alikuwa akilipwa.
 
Mourinho ambaye ni kocha wa zamani wa Chelsea, Manchester United, Porto na Real Madrid anatazamiwa kuanza kibarua chake ugenini katika pambano dhidi ya West Ham leo Jumamosi na tayari amedai msimu huu utakuwa mgumu kwa timu yake kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini ujao anaweza kutwaa taji hilo.
 
Nisingeweza kuwa na furaha kubwa zaidi ya hii (kuchaguliwa kuwa kocha wa Tottenham), kuhusu kazi ngumu inayonikabili mbeleni kila timu ambayo inafanya mabadiliko katikati ya msimu inafanya hivyo kwa sababu hali ni mbaya, kwa hiyo hilo lipo wazi, labda kitu cha ajabu sana kitokee,” alisema Mourinho.
 
Kimsingi wakati mwingine matokeo yanalazimisha maamuzi haya. Hata hivyo, klabu hii ina kila sababu ya kufanya vyema. Wachezaji wanaonekana kuwa wazuri, nina furaha kwamba hiyo ilikuwa moja kati ya sababu ya mimi kuja hapa na Mwenyekiti Levy aliniwekea mezani wachezaji wazuri mbele yangu.”
 
Katika mechi 10 za mwanzo za Mourinho mara baada ya pambano dhidi ya West Ham anatazamiwa kurudi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Novemba 26 wakati Spurs itakapoikaribisha Oliympiakos katika pambano linalotarajiwa kuwa lake la kwanza nje ya ligi akiwa na timu hiyo.
 
Novemba 30, Spurs itacheza na Bournemouth nyumbani lakini siku nne baadaye, Desemba 4, Mourinho atasafiri mpaka Old Trafford kuikabili timu yake ya zamani, Manchester United katika pambano lake la kwanza uwanjani hapo tangu afukuzwe Desemba, mwaka jana.
 
Desemba 7, Spurs itacheza na Burnely ugenini na Desemba 11 itacheza dhidi ya Bayern Munich ugenini katika pambano la Ligi ya Mabingwa. Pambano la awali lililofanyika London Spurs chini ya Pochettino ilikubali kichapo cha mabao 7-2 nyumbani.
 
Back
Top Bottom