Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yaani kamwe sitatembea pekeyangu [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Pambana nao mi nasubiri niku sapot.
Yaani haupo peke yako[emoji23][emoji23]
Halafu Hawa hata wangekuwa wote bado hawanizidi Hawa[emoji3]na hivi tumeshinda[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ramadhan Ibrahim Saadalla
Huyu alikuwa mtoto wa kaka yake Saleh Saadalla aliyekuwa waziri katika Serikali ya Mavamizi Zanzibar. Ramadhan alipofungwa alikuwa na umri wa kiasi cha miaka 40 mpaka 45. Siha yake ilikuwa nzuri ingawa naye kwa mujibu wa maelezo yake, alisema kuwa aliteswa sana alipokuwa katika gereza la "Kwa Ba Mkwe".

Ramadhani alisononeka kwa wakati mkubwa akiwa hapo hapo juu ya kirago chake katika gereza la Langoni. Alipofika katika sakaratilmauti, ndipo alipoondoshwa na kupelekwa huko huko kwenye hicho kihospitali cha Makao Makuu ya Magereza, Kiinua Miguu.

Naye wakati wake ulipofika, aliondoka kama waliyomtangulia. Hawa ndio niliyowaona mimi tu kwa nafsi yangu wakiachwa wakiatilika na maradhi bila ya matibabu mpaka wakafa hali wanajiona. Nina hakika wapo wengine wengi waliokuwa wametendewa kama hayo wakati wakiwa ni wafungwa wa kudhulumiwa na Karume pamoja na Serikali yake.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Jamanii,

Na badaae Man u akifungwa, utakuja ushangilie[emoji23][emoji23][emoji23][emoji2088][emoji2088]
Na hivi Mimi sio mgumu kulia,machozi yapo karibu[emoji23][emoji23]
Akinizomea tu na Mimi simuachi salama[emoji3] ,namkandika nalo kisogoni..najua nikikimbia hawezi kunikamata..ile milima ya tukuyu atanikutia wapi huyu mchovu tu Kama kitimu chake kiaseno[emoji23]
 
Naam
 
WAMEULIWA VIFUNGONI
AbdulAziz Twala, Idris Abdalla Majura
Wote wawili walikuwa miongoni mwa "wafungwa wa kisiasa" waliofungwa vifungo vikubwa vikubwa vya kuanzia miaka mitano hadi 10 bila ya kupelekwa mbele ya mahakama ya sheria na bila ya hata kupewa haki yoyote ya kujitetea. Wakati huo walipouliwa walikuwa wamesha vitumikia vifungo vyao kwa muda. Mwanzoni wa mwaka 1971, Twala na Majura walitoroka kutoka gerezani, Langoni. Kwa bahati mbaya usiku wa siku hiyo hiyo waliotoroka walipatikana na walikamatwa tena na kupelekwa gerezani "Kwa Ba Mkwe".
 
 
Huko waliteswa sana na baada ya kuteswa, waliuliwa wote wawili kwa kupigwa risasi. Kwa kuwa mimi (mwandishi wa kijitabu hiki) nilikuwa pamoja nao sana wakati tulipokuwa sote wafungwa wa Karume katika gereza la Langoni, Idara ya Usalama ilinichukua kutoka gereza la Langoni na nilipelekwa kwenye gereza la "Kwa Ba Mkwe" kwa kufikiria kuwa mimi ninaweza kuielewa mipango yao ya kutoroka gerezani na wapi walipokusudia kwenda. Kwa vile waliweza kuwakamata usiku huo huo, hawakuwa na haja tena na mimi.

Bali hata hivyo, niliwekwa katika gereza hilo la "Kwa Ba Mkwe" kwa muda wa siku 38. (Kuwekwa katika geraza hilo kwa muda wa mwezi, hata usifanywe chochote, basi afadhali uwekwe miezi miwili katika gereza la kawaida). Nilipokuwepo katika gereza hilo la "Kwa Ba Mkwe" mmoja katika wachungaji wa gereza hilo, alinino'goneza kuwa, "
Twala na Majura wameshapigwa risasi, na wote wawili wametumbukizwa katika shimo moja".
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hakuwezii kabisaa
 
WAFUNGWA WENGINE WAULIWA
Wananchi wafuatao walikuwa katika gereza la Langoni wakivitumikia vifungo vyao vya miaka kumi kumi walivyofungwa na Serikali ya Mavamizi. Jaha Ubwa Mdungi Usi Juma Maulidi (Jimmy Ringo) Khamis Masoud Aboud Nadhif

Mwaka huo huo wa 1971, mwaka waliouliwa Twala na Idris Majura, kiasi cha saa moja unusu ya usiku wananchi hao wote watano walichukuliwa kutoka gerezani. Kutoka siku hiyo hadi hii leo hawajaonekana tena, na wala hawataonekana katika ulimwengu huu. Siku ya taarikh 9 Januari 1972, Karume na gengi lake la Baraza la Mavamizi walikuja gerezani Langoni kuwaachilia huru wafungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…