Yesu wa Tongareni anasema, familia yake haikuipokea vyema taarifa ya kubadilisha jina na kuitwa Yesu na kuacha mienendo yake ya zamani.
'Wengi walinena huyu ameharibika kichwa, huyu ni mwendawazimu, hata amerukwa na akili na anaongea lugha zisizoeleweka'' alisisitiza yesu wa Tongareni ambaye alisema anaamini akili yake iko sawa kulingana na mapenzi ya Mungu.
Aliwaomba watu wawe kati toba ili waokolewe, akiamini kuwa katika jiji la Naoirobi ni watu wawili tu watakaookolewa siku ya mwisho( ya kiama).