Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

i mara ya kwanza kwa eneo la magharibi mwa kwa watu Kenya kujitambulisha kuwa na uwezo wawakuaminiwa kiimani.

Katika miaka ya nyuma mwanamume mmoja magharibi mwa Kenya aliyejiita Jehova Wanyonyi alidai kuwa yeye ndiye Mungu.

Alikuwa na waumini na alikuwa ameoa wanawake zaidi ya wanawake 10 na watoto zaidi ya 100.

Wake zake pamoja na watu wengine watano waliomzingira wakati wote walijiita malaika.
1575517323368.png
 
Hata hivyo kiongozi huyo wa madhehebu wa kundi linalojiita Waisraeli, alipotea na baadae serikali ya Kenya ilitangaza kuwa alifariki na wafuasi wake kuzika maiti yake mahali pasipo julikana.

Hata hivyo wafuasi wake walisema kuwa Jehova Wanyonyi bado yu hai na anaendelea kufanyiwa matibabu katika hospitali moja nchini ingawa hawajui ni ipi.
 
Masharti ya kuingia katika mashindano ya Mrembo wa Dunia yana ubaguzi …hakuna nafasi yake katika karne hii ya 21''
Mrembo Veronika Didusenko mwenye umri wa miaka 24, alishinda taji la mrembo wa Ukraine (Miss Ukraine) mwaka 2018 lakini alinyang'anywa taji hilo pale waandaaji walipogundua kuwa ni mama.
 
1575517500613.png


Sheria za shindano zinapiga marufuku mrembo yoyote kushiriki katika mashindano yatakayoruhusu kushiriki katika mashindano ya mrembo wa dunia kama wakiwa na watoto.
Na sasa Veronika, ambaye ana mtoto mwenye umri wa miaka 5, ameamua kuchukua hatua za kisheria kwa waandaji wa mashindano hayo kuhusu sheria zao.
 
'Nataka niwabadilishe, na kuwapa changamoto. Nataka nihakikishe sheria za kushiriki mashindano ya urembo wa dunia zibadilike na zilingane sawa sawa na wakati huu.'' Aliiambia Radio 1 Newsbeat.

'Nataka niwaweke sawa kutokana kwa maisha ya sasa na kuangalia maisha halisi ya wanake kwa nyanza hizi, na kutambua kuwa wanaweza kufanya kazi na vile vile mambo mengine nje ya kazi.'
 
Veronika anadai aliamua kushiriki Taji la ''Miss Ukraine'' kukuza kituo chake cha kusaidia watu na alishangaa alipopewa ushindi wa shindano hilo.
Angeenda kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya urembo wa dunia lakini siku nne baadae alinyang'anywa taji hilo.
'' Ilikuwa ni jambo la aibu na la kufedhehesha kwangu,'' alisema.
 
Nilijisikia vibaya kwasababu sio mimi peke yangu ninayofanyiwa haya, ni kitu ambacho wanawake wengi duniani wanakabaliana nacho, ambao labda wanataka kushiriki lakini hawaruhusiwi kushiriki kwasababu tu wana watoto.''

Veronika amekubali kuiona shetia hiyo kwenye fomu ya kuomba kushiriki, lakini alishauriwa kushiriki na waandaji hao.

''Kwanini mwanamke akataliwe kushiriki kwasababu tu ni mama? Haitii maanani kabisa''

''Kuwa mama haileti madhara yanayomzuia mshiriki kufanya kazi au kuwa mwanamitindo au kufanya kazi zangu.''

''Kwahiyo sheria hizo hazikuleta maana yoyote kwangu.''
 
Mwenyekiti na mkurugenzi mkuu wa shirika la ''Miss World'' Julia Morley, aliulizwa kuhusu sheria hiyo katika mahojiano mwaka jana.
''Unapojaribu shirika la kimataifa likubaliane na wewe, inabidi uangalie kila mtu na wanapiga kura kulinagana na yale yaliyoruhusiwa.'' Aliiambia Good Morning Britain.
 
Ndani ya mwaka 2014, kiongozi wa shindano la urembo nchini Uingereza lijulikanalo kama 'Miss England competition' Angie Beasley, alisema itakuwa ngumu sana kwa washindi kugawanya muda wao kwa kazii hii ya urembo na kuwa mama.
Akizungumza na kituo cha habari cha ITV Bi Angie alisema ''Kitendo cha mama kusafiri sehemu mbali mbali duniani akisaidia vituo vya kutoa misaada kwa watoto kwa mwaka mmoja, ni jambo halimtendei haki mtoto pamoja na familia nzima.''
 
Veronika anasema anatumaini kuwa kitendo cha yeye kuchukua hatua ya kisheria kutawafanya 'Miss World' kubadilisha sheria hiyo. Shindano hilo linaanza mwaka huu mjini London tarehe 14 Disemba.

Anawakilishwa na mwanasheria wa kutetea haki za kibinadamu Ravi Naik ambaye anadai chini ya sheria ya haki swa ya mwaka 2010, sheria hiyo ya kuingilia shindano hilo ni ya ubaguzi.
 
Mashindano ya ulimbwende nchini Tanzania mwaka 2014 yaliingia dosari la namna hiyohiyo kwa madai ya udanganyifu wa kuwa na mtoto na hivyo kuvuliwa taji la Tanzania kwa mwaka huo.
Bi Basila Mwanukuzi ambaye aliwahi kuwa Mlimbwende wa Tanzania 1998 na sasa ni muandaaji wa mashindano hayo hakutaka kuzungumzia suala hilo la kuwa kile kilichotokea Ukraine kiliwahi kutokea nchini mwake, "sikuwa kiongozi wakati huo hivyo sijui chochote, "
 
Back
Top Bottom