Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kisa Harry Kane ameumia. Ripoti zinadai straika huyo chaguo la kwanza kwenye fowadi ya Tottenham huenda akawa nje ya uwanjani mwezi mzima baada ya kuumia misuli ya nyuma ya paja kwenye mchezo dhidi ya Southampton juzi Jumatano.
 
Jambo hilo lilimfanya Mourinho kuonyeshwa kadi ya njano.
Filimbi ya mwisho ilipopulizwa, Spurs ilikuwa imechapwa 1-0, Southampton ikipata ushindi wake wa tatu katika mechi nne za mwisho. Lakini, kipigo hicho kilikuwa kigumu kwa Mourinho, kwa sababu wamechapwa mara ya pili katika mechi nne za mwisho.
 
Kukosa huduma ya straika huyo muhimu hasa kwenye kipindi hiki ambacho Mourinho anapambana kuhakikisha Spurs inamaliza ligi ndani ya Top Four, anaweza kushawishika kuingia sokoni Januari kunasa huduma ya straika mpya kuja kuja kufanya kweli kwenye kikosi hicho.
 
Spurs imekuwa na wigo finyu wa uchaguzi kwenye safu yake ya ushambuliaji baada ya kumruhusu straika Mhispaniola, Fernando Llorente kuondoka bure kwenda kujiunga na Napoli kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi.
 
Son Heung-Min na Lucas Moura walitumika kama washambuliaji wa kati huko nyuma na Kocha Mauricio Pochettino wakati Kane alipokosekana uwanjani kutokana na matatizo mbalimbali. Mourinho hana ujanja zaidi ya kufanya hivyo.
 
Levy hatakuwa na ujanja wa kumkwepa Mourinho kwenye hilo na pengine moyoni, kocha huyo Mreno atakuwa amefurahi kuumia kwa straika wake huyo namba moja kwa sababu jambo hilo litampa fursa ya kuleta jembe jipya kikosini.
Kwa wakati huu, straika kinda Troy Parrott atalazimika kuaminiwa na kupewa majukumu, basi Levy itabidi afungue pochi dirisha la Januari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…