Alvaro Negredo -miaka 34
Manchester City na Middlesbrough zitakuwa na kumbukumbu nzuri ya mshambuliaji Negredo, 34, ambaye alicheza kwenye timu nyingi sana za Ulaya na nje ya Ulaya. Lakini, staa huyo atakumbukwa vizuri zaidi huko Hispania, alipokuwa kwenye kikosi cha Sevilla, ambapo alicheza mechi 139 na kufunga mabao 70. Kwenye soka la kimataifa akiwa na kikosi cha La Roja, alifunga mabao 10 katika mechi 21, akionyesha kwamba yeye ni hatari katika kucheka na nyavu. Kutokana na hilo, klabu ya Al-Nasr Dubai SC ilimsainisha mwaka 2018. Amefunga mabao 22 katika mechi 29.